Home » » WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA

WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA

Serikali ya Mtaa wa Muheza katika halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kushirikiana na wananchi imeamua kujenga daraja kwa njia ya kujitolea ili kupunguza kero wanazopata kipindi cha msimu wa mvua.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Muheza BW. MOHAMED LINGOWICHE amesema wameamua kuchukua uamuzi kutokana na kero zinazowakabili kipindi cha mvua na kusababisha maisha ya wananchi kuwa hatarini.

BW.LINGOWICHE ameongeza kuwa kinachosaidia katika ujenzi huo wa makaravati ni kutokana na wananchi wake kuwa wenye kuzingatia mambo na kumuelewa pale alipoitisha kikao cha wananchi kuwaelezea kusudio la wananchi kujitolea kujenga makaravati hayo.

Amefafanua kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha, BW.SYLVESTER KOKA ametoa shilingi laki sita na wananchi wakichangia shilingi laki 2, na kuwezesha kuchongwa kwa barabara hiyo inayounganisha mtaa huo.

\Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara Mtaa wa Muheza, BW. ASHRAF MMARI amesema mpaka sasa ujenzi wa Makaravati umegharimu shilingi milioni 3.5,ili kuweza kukamilisha ujenzi huo ambao jumla ya makaravati 9 yenye kipenyo cha mm 90, na hivyo kuwezesha wananchi kupita kwa muda wote.


BW.MMARI amefafanua kuwa wamekuwa wakipata michango mbalimbali ya fedha na vitendea kazi, wakati mafundi wanaojenga makaravati hayo ni mafundi ambao wanaishi nao mtaani na hivyo kurahisisha kwa kiasi kikubwa kazi hiyo ya kujitolea.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa