Naibu
Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu mwenye kitambaa chekundu kichwani
,akiwa ameambatana na mbunge wa jimbo la Bagamoyo.dk.Shukuru Kawambwa wa
pili kushoto na wengine ni viongozi mbalimbali wa kijiji cha Kongo na
kata ya Yombo wakati alipokwenda kutembelea maeneo yanayotekelezwa mradi
wa umeme vijijini (REA )awamu ya III ,ambapo amejiridhisha na kasi
anayoendelea nayo mkandarasi Sengerema.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Nguzo
60 za umeme zilizotelekezwa ndani ya miaka mitatu huko kijiji cha
Visezi Kata ya Vigwaza pasipo kufanyiwa kazi ,jambo linaloelezwa ni
uzembe uliofanywa na mkandarasi MBH aliyepewa kazi awamu ya pili ya
mradi wa umeme vijijini (REA )ambapo ameitia hasara serikali na
kuchelewesha huduma ya umeme kwa jamii(picha na Mwamvua Mwinyi)
Naibu
Waziri Wa Nishati ,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Visezi kata ya Vigwaza kuhusiana na masuala ya huduma ya umeme.
Na Mwamvua Mwinyi-Bagamoyo
NAIBU
Waziri Wa Nishati Subira Mgalu, ameridhishwa na kasi na kazi
anayoendelea nayo ,mkandarasi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya
III, Sengerema huko kijiji cha Kongo na kata ya Yombo wilaya ya Bagamoyo
,Mkoani Pwani.
Aidha
amelitaka shirika la umeme (Tanesco) wilaya ya Bagamoyo, kukimbizana na
wakati kwa kuwapa wananchi fomu za kujaza ili kupatiwa umeme wakati
zoezi la kuweka nguzo likiendelea katika baadhi ya vijiji.
Aliyasema
hayo wakati alipokwenda kutembelea kijiji cha Kongo ,kata ya Yombo na
Visezi kata ya Vigwaza na kujiridhisha na kazi ya mradi huo
inavyoendelea .Mgalu alisema mkandarasi huyo ameahidi kumaliza kazi hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao na kwa uhakika anakwenda vizuri.
Alieleza kwasasa amekuta wanaendelea na kazi ya kusimamisha nguzo na maeneo mengine yanatarajiwa kutandaza nyaya ."Mkandarasi
Sengerema yupo Mkoa wa Iringa na Pwani ,ameanza kazi vizuri na ndivyo
tunavyohitaji ,tunaomba aendelee na kasi hii ili wananchi wapate huduma
hii ya umeme haraka" alisisitiza Mgalu.
Naibu
waziri huyo,alitoa tahadhali kwa wakandarasi wengine wa mradi wa REA
kwenda na kasi inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano,na atakaefanya
kazi chini ya kiwango hatakuwa na masihala nae.
Pamoja
na hayo ,alilitaka Shirika la Umeme (TANESCO) mkoani Pwani,kwenda
kuhakiki nguzo 120 zilizotelekezwa chini miaka mitatu mfululizo,.kwenye
vijiji hivyo ,ili kujua kama bado zinauwezo wa kutumiwa
Mgalu
alisema, nguzo 60 zilizopo kijiji cha Visezi na nguzo nyingine 60 kijiji
cha Kongo ,zilipelekwa na mkandarasi MBH kwa maelekezo ya umeme
vijijini (REA)awamu ya II ,ambae alifanya uzembe .
Alieleza
,Tanesco ihakikishe inahakiki nguzo hizo bila kufanya ajizi kwani
serikali ilishamlipa fedha mkandarasi huyo awamu iliyopita ,hivyo
itakuwa ni hasara kubwa kuziacha nguzo hizo pasipo kuzifanyia kazi .Mgalu
alisema mkandarasi huyo ,hatoshi na amechelewesha huduma ya umeme kwa
wananchi na atachukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa
wakandarasi wababaishaji na wazembe.
”Ninaomba
zikaangaliwe kama zinawezekana kufanyiwa kazi ,zitumike katika maeneo
ambayo zitafaa kupelekwa ,kuliko kuendelea kukaa chini na kusababisha
maswali ’alisema.
Mgalu
aliwaeleza wakazi wa Visezi kuwa kijiji hicho kinatarajia kupata umeme
kupitia mradi wa umeme unaotekelezwa katika mkoa wa Pwani na baadhi ya
maeneo jijini Dar es salaam ikiwemo Kigamboni (PERI-URBAN).
Nae
mbunge wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete ,alisema anaimani na
wizara ya nishati na nia nzuri ya serikali kwa kupeleka umeme katika
vitongoji vyote na hakuna kitongoji kitakachoachwa.
Alisema
,kijiji cha Visezi kimezungukwa na fursa za chama cha ushirika cha
umwagiliaji,gesi,ukaribu wa bandari kavu ya Kwala ,hivyo kinapaswa
kupatiwa huduma ya umeme ili kunufaika na kuinua uchumi wake.
Ridhiwani
,alieleza ni wajibu wa wakandrasi na Tanesco kufanya kazi inayotarajiwa
na jamii ili kuwaletea maendeleo wanayoyategemea .Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Kongo,waliipongeza serikali kwa kuwasogezea
huduma ya umeme karibu na wanaamini maendeleo yataongezeka.
0 comments:
Post a Comment