Muonekano
wa leo wa tuta la kutandazia reli ya kisasa (Standard Gauge) katika
eneo la Soga mkoa wa Pwani takriban kilomita 37 kutoka Pugu mkoa wa Dar
es salaam ulivyo sasa, ikiwa ni hatua iliyofikiwa katika muendelezo wa
ujenzi wa reli hiyo ulioanza mwezi Desemba mwaka jana katika mradi
unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu na utajengwa kwa awamu
nne.
Kampuni
Hodhi ya rasilimali za reli nchini (RAHCO) ndiyo inatekeleza mradi huo
kutoka Dar es salaam kwenda Isaka na Mwanza imegawanyika katika awamu
ndogo nne ikiwemo Dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora,
Makutupora hadi Tabora na Tabora hadi Mwanza.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Injinia Masanja Kadogosa jumla
ya makandarasi wanne wanaendelea na kazi usiku na mchana ili
kukamilisha ujenzi wa reli hiyo yenye upana wa mita 1.345 na ambao
utaruhusu treni kutembea kwa spidi ya kilomita 160 kwa saa. Mradi huu
mkubwa unatarajiwa kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo,
biashara, madini na viwanda hususan maeneo ambapo reli hiyo itapita
ikiwemo nchi jirani ya Rwanda ambayo imekubali kujenga aina hiyo ya
reli toka Isaka hadi Kigali.
Mtandao
mzima wa reli nchini unaotegemewa kujengwa kwa kiwango cha standard
Gauge una jumla ya kilometa 2,561 ukitarajiwa kugharimu Dola za Marekani
Bilioni 7.683.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment