Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel
Mjema(kushoto) akizungumza na viongozi na baadhi ya watumishi wa
Hospitali ya wilaya ya Kisarawe leo kabla ya kukabidhi msaada wa shuka
176 kusaidia wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
Aron Msigwa -MAELEZO.
[Kisarawe, PWANI]. Wito
umetolewa kwa Taasisi, mashirika na makampuni kote nchini kujenga
utamaduni wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata katika kuisaidia jamii
kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Wito
huo umetolewa leo mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara
Dar es salaam Prof.Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa shuka 176
zilizotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya
wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.
Amesema
CBE mwaka huu imetimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1965,
hivyo ukongwe na umri wake nchini Tanzania umekua ukiendana
na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea ndani na nje ya nchi ili kukidhi
mahitaji na matarajio ya watanzania.
“CBE
tukiwa chuo kikongwe nchini tumefanya mengi yenye manufaa kwa uchumi wa
nchi yetu na jamii ya watanzania,kwa kuwathamini wananchi
tunaowahudumia tuna utaratibu wa kurudisha sehemu ya faida tunayoipata
kwa jamii na mwaka huu tulitenga kiasi cha shilingi milioni 9 kusaidia
wodi za wazazi katika hospitali zetu” Amesisitiza.
Ameeleza
kuwa ndani ya miaka 50, CBE imewanufaisha wananchi na kutoa mchango
mkubwa katika maendeleo ya taifa kupitia Fani za Biashara, Ugavi na
manunuzi, Vipimo, TEHAMA , Utawala katika biashara pamoja na kutoa
huduma mbalimbali kwa jamii.
Amesisitiza
kuelekea miaka 50 ijayo chuo chake kimeelekeza nguvu katika kuwekeza
kwenye ubora na ujuzi wa kumuwezesha muhitimu kuitumia elimu aliyoipata
kuleta manufaa na mabadiliko katika jamii inayomzunguka.
“Sisi
kama chuo cha Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa
wataalam wenye ujuzi wa Biashara ndio maana tumeanza kufuandisha
wanafunzi wa Shahada ya Elimu katika Biashara ili tupate wahitimu bora
watakaokidhi mahitaji ya soko” Amesisitiza.
Kwa
upande,Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Martin Msokela akizungumza mara
baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo,
ameushukuru uongozi wa CBE kwa kuwakumbuka wagonjwa wa Hospitali ya
wilaya ya Kisarawe.
Amesema
msaada uliotolewa na chuo hicho umepunguza uhitaji wa mashuka waliokuwa
nao kwani Hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo la uhaba wa mashuka
kwenye vitanda vya wagonjwa.
Dkt.Msokela
amewaomba wadau wengine kujitokeza kwa wingi kuisaidia hositali hiyo
kama walivyofanya CBE ili kuboresha afya za wagonjwa wanaofika
hospitalini hapo kutibiwa.
”
Nawaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia kama walivyofanya CBE, licha
ya hili la mashuka ukiangalia Jiografia ya Kisarawe,Hospitali yetu
imekua na tatizo la upatikanaji wa maji na uchakavu wa mitambo”
Amebainisha.
Aidha
katika hatua nyingine Dkt.Msekela ameeleza kuwa hali ya ugonjwa wa
Kipindupindu wilayani humo inaendelea kudhibitiwa kupitia timu ya
wataalam iliyoundwa kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa
hospitali hiyo imepokea mgonjwa mmoja mwenye tatizo hilo.
Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokela akiongea na watumishi wa
hospitali ya wilaya ya Kisarawe kabla ya kupokea msaada wa mashuka ya
wagonjwa wilayani humo leo. Mashuka hayo yametolewa na chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es Salaam (CBE).
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akikabidhi
msaada wa shuka 176 kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya
Kisarawe Dkt. Martin Msokela (kulia) leo. Mashuka hayo yametolewa na
chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali hiyo iliyokuwa
ikikabiliwa na uhaba wa mashuka.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akikabidhi
msaada wa shuka 176 kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya
Kisarawe Dkt. Martin Msokela (kulia) leo. Mashuka hayo yametolewa na
chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali hiyo iliyokuwa
ikikabiliwa na uhaba wa mashuka.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(katikati), Kaimu Mganga
Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokelo(kulia) na
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed Mzige kwa pamoja
wakitandika sehemu ya msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na CBE
kwenye wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(wa pili kushoto), Kaimu
Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin
Msokelo(kushoto ) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed
Mzige (kulia) na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Kisarawe wakielekea
lilipo jengo la wodi ya wazazi.
Wauguzi wa Hospitali ya
wilaya ya Kisarawe wakifurahia msaada wa mashuka yaliyotolewa kwa
wagonjwa na Chuo cha Elimu ya Biashara, CBE leo.( Picha zote na Aron
Msigwa – MAELEZO).
0 comments:
Post a Comment