Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
SERIKALI
mkoani Pwani, imeitikia wito wa serikali ya awamu ya tano ya kujenga
viwanda vya madawa na baadhi ya vifaa tiba ambapo inatarajia kuwa na
viwanda hivyo vitatu hali itakayoondoa adha ya kuagiza madawa nje ya
nchi .
Aidha
imekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wawekezaji ya kutoa ajira kwa
watu kutoka nje ya nchi na kuwabania fursa hiyo wanaPwani ama
watanzania.
Akielezea
masuala ya uwekezaji na ajira ,wakati wa ziara yake ya kutembelea
viwanda mjini Kibaha ,mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo
alisema Viwanda vya madawa vitawezesha kuokoa mamilioni ya fedha
yaliyokuwa yakitumika kununulia madawa nchi jirani na nje.
Alieleza
viwanda vitatu vinajengwa Mkoani Pwani ikiwemo Kairuki Pharmaceuticals
industry Ltd ,Zinga pharmaceuticals ambacho kitajengwa kwa ubia na
waislael na kipo mbioni kuanza kujengwa na Bahari pharmaceuticals .
"Tunaikitia
wito wa rais Dk.John Magufuli ,lakini pia tangu kipindi cha nyuma
tumejipanga kujenga viwanda hivyo ,kupitia ziara hii tunawathibitishia
wananchi tunaunga mkono kauli ya serikali yetu"alifafanua Ndikilo.
Pamoja
na hayo ,mkuu huyo wa mkoa alieleza ,zipo fursa mbalimbali za
uwekezaji lakini vijana na wazawa wanashindwa kukimbilia fursa hizo.
Ndikilo alisema wazazi na vijana bado hawajatambua kujipanga kukuza elimu na ujuzi wao kwa ajili ya kujipatia ajira kirahisi.
Alitoa rai kwa wawekezaji ,kuacha kuwanyima ajira wazawa na watanzania ambao wanaujuzi na sifa za kufanya kazi .
"
Haiwezekani tunajenga viwanda vingi lakini vijana ,waTanzania na
wanaPwani hawanufaiki na ajira zinazopatikana,haikubaliki"alisisitiza
Ndikilo.
"Sidhani
kama Pwani ama Tanzania nzima haina wenye sifa na ujuzi,hivyo aliwataka
wawekezaji hao watoe kipaombele kwa watanzania wenye uwezo .
Ndikilo
alisema amepokea taarifa uwekezaji wa standard gauge eneo la Soga
hawatoi ajira hata ya udereva jambo ambalo analichunguza na atakapopata
uhakika watachukua hatua zinazostahili.
Aliwataka
kununua vifaa vya ujenzi kama nondo ndani ya nchi ,kwani taarifa
waliyompatia kwenye ujenzi wa Kairuki Pharmaceuticals industry Ltd kuwa
wananunua nondo huko Uturuki .
Alisema kipo kiwanda cha Kiluwa ambacho kinatengeneza nondo zenye ubora hivyo wanunue katika viwanda vya ndani ya nchi.
Nae
mkurugenzi mtaalamu wa Kairuki Pharmaceuticals eng.Valency Assenga
alisema ujenzi wa mradi huo ulianza machi 10 mwaka huu na mkandarasi ni
Petra Construction Ltd Ltd na unatarajiwa kumalizika Novemba 2018.
Alielezea
kazi zote zinaendelea kwani zipo hatua ya awali ya ujenzi na mpaka
kukamilika ujenzi wa awamu ya kwanza kiwanda hicho kitagharimu bilioni
3.9 " #
Eng
.Assenga alitaja changamoto kuwa ni miundombinu ya barabara,mradi
kusuasua kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na ucheleweshwaji wa
uunganishwaji wa umeme.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Mji huo ,Jennifer Omolo akizungumzia suala la mipango
miji alisema wameanza zoezi la kupima mji muda mrefu na wanaendelea na
zoezi hilo .
Omolo
aliwataka watu waache kujenga na kufanya biashara kiholela bila kupangwa
,na kuwashauri waone watalaamu wa mipango miji ofisi ya mkurugenzi ili
kupewa maelekezo ya kupata vibali .
0 comments:
Post a Comment