Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu wa Waziri na Uvuvi, Abdallah Ulega akipokea taarifa ya ujenzi wa Zahanati ya Sunguvuni mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo ,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani.
Meneja wa Tarura,Peter Shirima akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa barabara.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Ally Msikamo akizungumza juu ilani ya CCM na wananchi wa Sunguvuni mkoani Pwani.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Wananchi wa unguvuni mkoani Pwani wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
Muonekano wa jengo la Zahanati ya Sunguvuni mkoani Pwani.
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema miundombinu ya
barabara za vijiji ikijengwa itafanya vijiji kuinuka kiuchumi.
Ulega
aliyasema hayo wakati alipokutana na wananchi wa kijiji cha Singuvuni
kata Mkuranga wilayani Mkuranga, kuwa taasisi ya barabara za vijijini
na Mijini Tarura ni suluhisho kwa barabara za vijijini.
Amesema kuwa wananchi wa sunguvuni wanachangamoto ya barabara ambapo changamoto hiyo itatatuliwa na Tarura katika wilaya ya Mkuranga na hatimaye wananchi wataweza kuinuka kiuchumi kutokana na miundombinu hiyo.
Katika
ziara hiyo ametoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati
ya Sunguvuni pamoja na kuahidi mifuko 20 ya Saruji ili ujenzi huo uende
kwa kasi
Aidha amesema kuwa wanachi Sunguvuni wafanye kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo kutokana na kuwa na ardhi yenye Rutuba.
Meneja wa Tarura wilaya ya Mkuranga,Peter Shirima amesema wameshatenga milioni 18 kwa ajili ya kushughulikia sehemu korofi na amesema barabara zote wameshazipitia na kilichobaki ni utekelezaji.
0 comments:
Post a Comment