Home » » MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Picha zote na Elisa Shunda
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Mlao (kulia) wakielekea kupanda ndege kuanza safari kuelekea wilayani Mafia.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao (kulia) wakiwa ndani ya ndege safarini kuelekea wilayani Mafia kwa ziara ya kutembelea umoja wa vijana.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani, Ramadhan Mlao wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mafia tayari kuanza kwa ziara yao.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akilakiwa na mwenyeji wake Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mafia tayari kuanza kwa ziara yake.

Wenyeji wakiwaongoza wageni kutoka nje ya uwanja wa ndege wa Mafia.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia,Gilbert Sandagula akitoa ufafanuzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri kwa ujumla jinsi inavyosaidia vijana wa wilaya hiyo kunufaika na mikopo na miradi mbalimbali inayotolewa na ofisi hizo kwa vijana. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akiulizia mambo mbalimbali yahusuyo vijana wa Wilaya ya Mafia kwa uongozi wa wilaya hiyo ofisini hapo. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango,akizungumza wakati Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao walipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia kupokea taarifa ya usaidizi wa ofisi hiyo katika kuwasaidia vijana wa wilaya hiyo kwenye mikopo ya asilimia 4%.
Katibu wa Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani,Fakh Seif akizungumza na akielezea masuala mbalimbali yanayofanywa na mbunge wa jimbo hilo katika kuwasaidia vijana wa wilaya ya Mafia.


Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM),Amina Tuki akizungumza katika mkutano huo na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa chama hicho.


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo. Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM), Ally Omary Hassan akikabidhi risala ya umoja huo kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (Kulia) katika mkutano na wajumbe wa baraza UVCCM la wilaya ya Mafia. Anayeshuhudia Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM),Amina Tuki
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Mlao akiwasisitiza wajumbe wa baraza la UVCCM Wilaya ya Mafia kwa kushirikiana na viongozi wao katika kuhakikisha wanaimarisha chama hicho ili kishinde kwa kishindo uchaguzi ujao wa serikali za mitaa ambao ndiyo sahihi ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia (UVCCM),Amina Tuki. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki (kushoto) vitabu vya kanuni 100 na kadi za umoja wa vijana 200 kama zawadi kwa ajili ya jumuiya hiyo ya vijana ya Wilaya ya Mafia. Wanaoshuhudia kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (aliyejifunika kitambaa rangi ya njano) na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,,Ramadhan Mlao (kushoto kwake) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia. Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia,Mohamed Faki (kushoto) baada ya kumalizika kwa shughuli za mkutano na wajumbe wa baraza la vijana la UVCCM la Wilaya ya Mafia. 
 Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mafia,Mohamed Faki (kushoto) baada ya kumalizika kwa shughuli za mkutano na wajumbe wa baraza la vijana la UVCCM la Wilaya ya Mafia.


 
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (aliyejifunika kitambaa rangi ya njano) na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,,Ramadhan Mlao (kushoto kwake) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia.





Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro.




Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao akibarizi na kujionea uzuri wa fukwe za bahari katika Kisiwa cha Mafia.




NA ELISA SHUNDA,MAFIA .

VIONGOZI wanaounda Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mafia wametakiwa kujitoa kwa nguvu,mali na rasilimali zao katika kukitumikia chama hicho na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu 2020 ili CCM katika wilaya hiyo kiibuke na ushindi wa kishindo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Charangwa Selemani Makwiro wakati alipofanya ziara wilayani humo leo ambapo katika kuhakikisha vijana wa wilaya hiyo wananufaika na serikali ya Dk.John Pombe Magufuli amepata fursa ya kutembelea ofisi ya wilaya na halmashauri ambapo amekutana na uongozi na kupewa maelezo ya mnufaiko wa vijana wa Mafia katika asilimia 4% ya mikopo na miradi inayotolewa na uongozi huo kwa vijana hao.

Mwenyekiti Makwiro amewaeleza vijana hao kuwa wao ndiyo nguvu ya chama na kuwataka kusimama ngangari kama viongozi na vijana wa CCM kwa kutumia nguvu,mali,akili na rasilimali zao zote katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwakani wa serikali za mitaa ambapo ndiyo msingi wa ushindi wa uchaguzi mkuu wa madiwani,ubunge na urais hivyo ni jukumu lao vijana kukipigania chama katika maandalizi ya uchaguzi huo.

“nimefarijika siku ya leo kukutana na viongozi na vijana wa CCM wa Wilaya hii ya Mafia napenda kuwausia na kuwakumbusha vijana wenzangu mmeomba nafasi za uongozi kwenye maeneo yenu hivyo basi unapoomba nafasi katika chama hiki usitarajie labda kuna hela utapata au uwe kibaraka wa kiongozi Fulani ili maisha yako yaendelee hapana umeomba nafasi ya uongozi kwa ajili ya kuwatumikia vijana wenzako ni jukumu lako kama kiongozi sasa kutumia nguvu zako,akili,mali na rasilimali katika kukitumikia chama hiki;

“Kupitia nyie vijana wa Chama Cha Mapinduzi ambao leo hii ni viongozi wa UVCCM kuanzia ngazi ya wilaya,kata na mitaa kuhakikisha mnakisaidia chama hiki kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa 2019 wa serikali za mitaa ambapo ushindi wa kishindo wa CCM ndiyo utakaowezesha maandalizi ya ushindi wa kishindo wa uchaguzi mkuu wa 2020 hivyo jitoeni kwa hali na mali mkisaidie chama hiki,msikubali kuwa watumwa wa watu katika kuwachagulia viongozi tumieni akili zenu katika kujitafutia kipato halali ili muwe na jeuri kwa watu wanaotaka kuwaweka mifukoni” Alisema Makwiro

Aidha Mwenyekiti huyo amewasihi vijana hao kuwa na uvumilivu kusameheana kuondoa tofauti baina yao zilizopo ambazo zimetokana na uchaguzi wa ngazi mbalimbali za vijana wilayani humo kuwaomba waungane wakijenge chama kwa pamoja na kukivusha salama katika chaguzi zijazo za serikali ya mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Hata hivyo Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa PwaniRamadhan Mlao amewakumbusha vijana wa mafia kushirikiana katika ngazi zote kuhakikisha wanaijenga jumuiya ya vijana kwa kushirikiana kwa pamoja kuanzia ngazi ya shina hadi wilaya ili wakisaidie chama katika chaguzi zijazo.

Akizungumza kwa niaba ya vijana hao,Mwenyekiti waUVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki,alisema kuwa wamepokea maelekezo kutoka kwa viongozi hao yeye akishirikiana na wajumbe wa baraza la vijana wa wilaya hiyo kuhakikisha wanaitisha mkutano ili kuondoa tofauti zilizopo ambazo zilisababishwa kwenye kipindi cha uchaguzi.

Lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha kila mabaraza ya wilaya wanaelewa CBO kwa kina na ifanyiwe kazi kwa vijana kujiunga katika vikundi na kunufaika na fedha za vijana zinazotolewa na halmashauri husika ili kuinua uchumi wa vijana.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa