Home » » KATA YA MISUGUSUGU YAPATA OFISI ZA KISASA

KATA YA MISUGUSUGU YAPATA OFISI ZA KISASA

Katika kuonyesha kuwa maendeleo yoyote yanaletwa na wananchi, Kata ya Misugusugu mjini Kibaha imefanikiwa kupata ofisi ya kata yenye hadhi ya juu kufuatia juhudi zilizofanywa na viongozi na wananchi wa kata hiyo.


Diwani wa Kata ya Misugusugu ambaye pia ni mwenyekiti Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW. ABUDHADI MKOMAMBO amesema hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya kata ya Misugusugu iliyogharimu jumla ya milioni 45.


BW.MKOMAMBO amesema ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kujenga ofisi ya kata ambayo ipo katika kiwango cha kisasa na hivyo kurahisisha utendaji kazi wa viongozi wa Kata hiyo.

Mwenyekiti huyo wa baraza la halmashauri amebainisha mbali ya ujenzi wa ofisi hiyo ya Kata, kata yake imekuwa ikitekeleza miradi ya ujenzi wa ofisi za mitaa ambapo mpaka sasa wameshafanikiwa kukamilisha ofisi hizo kwa asilimia 90 katika mitaa 4 ya kata hiyo.

Akifungua ofisi hiyo, Katibu wa CCM ABDALAH MDIMU amesema kwamba ujenzi wa ofisi hiyo inaonyesha jinsi gani, Kata za mji wa Kibaha zilivyoamua kufanya kazi ya uboreshaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi.


BW.MDIMU ameongeza kuwa ujenzi wa Ofisi za kisasa katika kila kata kwa njia moja au nyingine zinaimarisha utawala bora, na kuimarisha utoaji huduma kwa jamii kwa kuwezesha kila kitengo kuwa na ofisi yake tofauti na hapo awali ambapo watumishi walikuwa wakitumia chumba kimoja.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa