Home » » Waethiopia 100 wakamatwa Pwani

Waethiopia 100 wakamatwa Pwani

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia raia 100 wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali katika matukio mawili tofauti.
Wahamiaji hao haramu walikamatwa saa 10:00 asubuhi Februari 17 mwaka huu, katika Kijiji cha Mwindu, Kata ya Ubena, Wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema kuwa wakati askari wakiwa doria, waliwakamata raia 33 wa Ethiopia wakiwa wamejificha kwenye msitu wa Magereza.
Alisema baada ya kukamatwa wahamiaji hao walipelekwa katika kituo cha polisi Chalinze wakisubiri taratibu za kisheria kuchukuliwa.
Katika tukio la pili, alisema kuwa Februari 18 saa 11:00 asubuhi, Waethiopia 67 walikamatwa wakiwa kwenye gari namba T 943 BET aina ya Fuso lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Samson (31).
Kamanda Matei alisema raia hao walikutwa eneo la Vikuruti, Kata ya Mlandizi, Wilaya ya Kibaha barabara ya Mlandizi Bagamoyo.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa