Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing mara baada ya kuweka jiwe
la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good
Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani. Kiwanda
hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vigae laki nane kwa siku na
mwekezaji ametumia zaidi ya Dola mil.50 katika uwekezaji huo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho cha vigae kilichopo Mkiwa
Mkuranga mkoani Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza
jambo wakati akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda
kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika
kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi wa Ikwiriri mkoani Pwani wakati alipokuwa akielekea mkoani
Lindi na Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku nne.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza
maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kiwanda hicho cha y Vigae cha Good
Will, Huang Heng Chao kutoka kwa Kiwandani hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
anapata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo kuhusu matumizi ya Gesi katika Kiwanda cha Vigae cha Good Will
kutoka kwa Kiwandani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia wananchi wa Somanga mkoani Lindi wakati akiwa ziarani
lkuelekea mikoa ya Kusini(Lindi na Mtwara).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF
katika eneo la Somanga wakati alipokuwa akielekea Nangulukulu katika
ziara yake ya mikoa ya Kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF
katika eneo la Nangulukulu, Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa katika ziara
ya mikoa ya kusini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Waziri
wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akifurahia hotuba iliyokuwa
ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli katika eneo la Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye mara
baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian
na mbunge wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya
kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
wananchi mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia
msaada wa Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni
mlemavu wa miguu katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye
shati la maua) ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha
(CUF) ambaye ameahidi kumpatia mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni
moja pia.
.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha
kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara
baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda
hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto
kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm
Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha
kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd leo
Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha
tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini
Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru
(kulia) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha
kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd, Robin
Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda
hicho leo Wilayani, Mkuranga.Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda
hicho jina lake(limehifadhiwa).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga
wananchi na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha
Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara
baada ya kuweka jiwe la msingi leo wilayani Mkuranga, Pwani.
Baadhi
ya wananchi wakitawanyika mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kuondoka baada ya
kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha
Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga, Pwani.
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment