Home » » MKE WA MUHESHIMIWA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA, MAMA TUNU PINDA ALA NONDOZ!

MKE WA MUHESHIMIWA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA, MAMA TUNU PINDA ALA NONDOZ!


 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisubiri kula Nondozzz jana kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria Kibaha. Mama Pinda nawasihi wanawake wote wajiendeleze bila kujali wako kwenye nafasi ipi kwani elimu haina mwisho. “Umuhimu wa elimu hauangalii kama wewe ni mke wa kiongozi au la, elimu inawahusu watu wote!,” alisema.
 
Alisema mahafali hayo yamempa hamasa ya kusoma tena zaidi na zaidi kwani ameona wahitimu wengine wakipata shahada za juu zaidi. “Nimeona wenzagu wakipokea Ph.D zao nikasema mimi nina Bachelor tu, hapana. Lazima niende mbele zaidi, Mama Tunu Pinda amefuzu nakupata shahada ya Uongozi wa biashara na biashara ya kimataifa (BBA_INTERNATIONAL BUSINESS) katika chuo kikuu huria Tanzania ambayo mahafali yake yamefanyika jana katika makao makuu ya yachuo hicho mkoni pwani
 Mama Pinda akiwa na mhitimu mwingine aliyejulikana kwa jina moja tu la Flora
 Mama pinda na wahitimu wenzie
Mama Pinda akipokea shada la maua toka kwa Mai Hazbendi wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa