Home » » AJALI YAUA 2 NA KUJERUHI 9, WAMO WAFANYAKAZI WA CRDB, TIGO

AJALI YAUA 2 NA KUJERUHI 9, WAMO WAFANYAKAZI WA CRDB, TIGO



Pwani

WATU wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka huko katika barabara kuu ya Bagamoyo Dar esalaam

Ajali hiyo imetokea leo Septemba mosi majira ya saa moja asubuhi na kwamba watu hao wawili waliopoteza maisha mmoja ni mfanyakazi wa Benki ya CRDB na mwingine ni mtumishi wa benki ya Akiba(Akiba bank) wote wakazi wa jijini Dar salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo Idrisa Shaban na Shida Mzee wakazi wa kijiji cha Matumbi Bagamoyo, wamesema ajali hiyo imehusisha gari T 845 ANB Toyota Hilux  na tukio hilo limetokea baada ya kupasuka gurudumu la mbele kushoto kisha kulivuta gari mtaroni na kupinduka.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei amethibitisha ajali hiyo na kutaja gari iliyohusika ni Toyota Hilux mali ya Paulo Mutaganjwa na kwamba ilikuwa ikiendeshwa na George Beda mfanyakazi wa kampuni ya Coca Cola.

Matei amesema katika tukio hilo watu wawili walikufa na tisa kujeruhiwa  na kwamba waliokufa ni William Temu (30) na Stella Godwin wote wafanyakazi wa benki hizo  na wakzi wa Dar salaam.

Matei amewataja majeruhi waliotambulika majina ni Vivi Mbwambo(27) mfanyakazi wa DSTV Mlimani City Dar esalaam, Neema Bernad(31) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mkoni ya TIGO Dar esalam, Godwin Bernad mfanyakazi wa Bandarini Dar esalam,

Wengine waliojeruhiwa ni dereva Beda, Glory Somi (30) mfanyabiashara, Hegela Nkya(34) mfanyabiashara, Joyce Muro(34) mfanyabiashara wote wakazi wa Dar salaam na wote walikuwa wakisafiri na gari hilo.

Kamanda Matei amesema majeruhi wote mara baada ya kuokolewa walipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya matibabu na kwamba miili ya marehemu hao nayo ilipelekwa kuhifadhiwa hapo.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa