Home » » FOLENI MIZANI: kero kubwa kwa wasafiri, madereva

FOLENI MIZANI: kero kubwa kwa wasafiri, madereva


Pwani

WASAFIRI wa magari ya abiria na madereva wa magari ya mizigo wamelalamikia kutumia muda mwingi kusafiri nyakati za usiku kutokana na kukumbana na foleni kumbwa katika maeneo ya Mizani wilayani Kibaha .

Wakizungumza jana mchana katika eneo hilo wasafiri hao wakiwemo madereva walisema eneo la mizani ya Kibaha imekuwa ni kama kanuni kukutana na foleni ambayo hata hivyo wamedai imekuwa ikichangiwa na baadhi ya askari wa usalama barabarani ambao huonekana eneo hilo wakitumia muda mwingi kufanya mazungumzo na madereva mazungumzo ambayo wao wanayatafsiri kama wanabembeleza kupewa kitu kidogo (fedha).

Husein Muhamed, Seif Anatori, Salum Mrisho, Mwamahamisi Mzao na Leila Almas wamesema katika vituo vyote vya mizani eneo la mizani Kibaha ndiyo inakuaga na askari wengi zaidi ya saba kila siku na kazi yao ni kukagua na kuhakikisha magari yanakuwa katika mpango mzuri lakini tatizo la foleni linakuwepo hivyo kushindwa kuelewa kazi wanayofanya askari hao kila siku kama ni kupunguza foleni ama jambo jingine.

Kufuatia malalamiko hayo,Afisa usalama barabarani mkoani humo, Nassoro Sisiwaya amekiri uwepo wa foleni mara kwa mara eneo hilo lakini amekanusha lawama zilizoelekezwa kwa askari wa usalama barabarani kutodhibiti hali hiyo kwa kusema kuwa uzembe wakati mwingine unasababishwa na madereva wenyewe kwa kufunga njia kwa haraka zao.

Sisiwaya pia amesema tatizo jingine kubwa ni magari makubwa, malori ambayo nyakati za jioni na asubuhi hutoka bandarini kwa wakati mmoja na kupelekea msongamano huo ambapo wanajitahidi kukabiliana nao na kudai kuwa kama
wakiacha kupanga askari hao eneo hilo hali itakuwa mbaya zaidi.

Hata hivyo amesema kwa sasa Serikali inaendelea na jitihada zake za kuondoa kero za foleni barabarani huku mchakato wa mizani ya Vigwaza Bagamoyo ukiendelea katika hatua za mwisho kukamilika na hivi karibuni mizani hiyo ikikamilika
itaondoa tatizo hilo linalolalamikiwa kwani magari mengine yatakuwa yakipima huko tu.



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa