Na Omari Mngindo, Bagamoyo
WANAMICHEZO watatu wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamefanikiwa kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa.
Wanamichezo hao ni John Bolizozo Katibu anayemaliza muda wake wa uongozi ndani ya Chama Cha Mpira wa Miguu wilayani hapa (BFA), Mousin Bharwan
mlezi wa timu zinazotoka ndani ya kijiji cha Vigwaza na Yussuf Kikwete mdau wa michezo Bagamoyo mjini.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Cha Sanaa na kusimamiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Abdul Marombwa, pia ulishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa na Katibu wa (CCM), Joyce Massi ambapo Bolizozo ameshinda nafasi ya Uenezi akiwaacha wapinzani wake Emmanuel Panduka na Kassim Gogo.
Bharwan ameibuka kidedea nafasi ya Mkutano Mkuu Taifa ambaye ameshinda nafasi hiyo kwa kujinyakulia kura 753 na kuwaongoza wenzake wane ambao ni Shumina Sharif, Yussuf Kikwete, Aeshi Khatibu na Issa Kibwana nao wamechaguliwa nafasi hiyo iliwaniwa na wagombea 15.
Wakizungumza baada ya matokeo hayo, Bharwan alianza kwa kuwashukuru wajumbe wa Mkutano huo kwa kuweza kumchagua na kwamba atatumia nafasi hiyo kuhamasisha michezo ikiwa ni kutekeleza ilani ya chama hicho.
“Katika Ilani ya chama chetu inagusia michezo, nitatumia nafasi hii kuhamasisha michezo mbalimbali ndani ya wilaya yetu kwa kuwapatia vijana fursa ya kimichezo kwani utakumbuka kuwa michezo kwa sasa ina
nafasi kubwa ya ajira,” alisema Bharwan.
Naye Bolizozo alisema baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya BFA akiwa Katibu atageuzia makali hayo katika nafasi ya Uenezi ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi nzuri ya kushiriki michezo sanjali
na kuhamasisha kujiunga na chama hicho.
“Nitatumia nafasi hii kuchagiza uendelezwaji wa michezo ndani ya Wilaya ikiwa ni kuunga mkono ilani ya CCM inayotaka kuendelezwa kwa michezo kwa wananchi bila kubagua itikadi za kisiasa,” alisema Bolizozo.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment