Mwandishi
wetu, Pwani
UONGOZI
wa bodi ya wakurugenzi katika shule ya awali na msingi ya Kibaha Independent
(KIPS) mjini Kibaha umesema unasikitishwa na vikwazo mbalimbali vya upatikanaji
wa eneo la ardhi vinavyowekwa na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya
mji huo ambapo kwa zaidi ya miaka minne sasa wamekuwa wakiomba kupatiwa
kwa ajili ya ujenzi wa sekondari lakini wamekuw awakipigwa dana dana tu.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa KIPS Alhaji Yusuph Mfinanga amesema wao kama
wawekezaji walikuwa na mpango wa kuendelea kujikita zaidi kwenye sekta ya
elimu lakini sasa wameanza kukata tamaa kutokana na kukosa eneo la kujenga
sekondari.
Alhaji
Mfinanga aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya shule hiyo kwenye
mahafali ya saba ya darasa la saba iliyofanyika katika eneo la Mkoani mjini
Kibaha.
Amesema
ni zaidi ya miaka nne sasa tangu uongozi wa shule hiyo ukiomba kupatiwa eneo la
kiwanja kwa ajili ya upanuzi wa shule hiyo pamoja na ujenzi wa Sekondari kwa
lengo la kuwekeza zaidi katika sekta hiyo lakini halmashauri hiyo imekuwa
ikiwazungusha licha ya kuwepo maeneo mengi yaliyopimwa ikiwemo lile eneo la
Tamco na mtaa wa machinjioni.
Mwenyekiti
huyo amesema tangu muda huo tayari shule imewasilisha maombi katika mamlaka
husika lakini bado hawajapata eneo hilo hali ambayo alisema inawarudisha nyuma
wao kama wawekezaji kwenye shughuli za maendeleo.
Aidha
Uongozi huo kwa mara ingine umeiomba Serikali ishirikiane nao kikamilifu katika
kuleta mapinduzi ya kielimu kwa kuwapa mawazo, ushauri na mchango wa hali na
mali ambao wataudhamini katika kufanikisha ukuaji wa maendeleo Kibaha
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment