na Julieth Mkireri, Kibaha
MBUNGE
wa Kibaha Mjini, Silvester Koka, amewataka viongozi na wanachama wa CCM
wilayani hapa kusitisha visasi na kupakana matope vilivyojengwa wakati wa
chaguzi za chama na badala yake wajipange kudumisha chama hicho.
Akizungumza
katika kikao cha kwanza cha Halmashauri Kuu CCM Wilaya ya Kibaha, Koka alisema
wanaCCM hawana budi kuanza kujipanga kwa muda mfupi uliobaki kabla ya uchaguzi
mkuu ujao bila kuweka mbele chuki zisizo na msingi.
Akizungumzia
wajibu wa viongozi mbalimbali, Koka alibainisha kila kiongozi ana wajibu wa
kutambua nafasi yake ya kazi bila kumwachia mtu mmoja afanye kazi za watu kumi,
hali inayosababisha wananchi kutupia lawama serikali ambayo haihusiki.
Aidha,
aliwaasa viongozi hao kuacha tabia ya kutoa siri za vikao vyao vya ndani
hususan vya kamati ya siasa, kwani kwa kufanya hivyo, ni sawa na kukibemenda
chama.
Naye
Katibu wa CCM Kibaha Mjini, Mwajuma Nyamka, alisema nguzo muhimu kwa sasa ni
wanachama kuwakubali viongozi wanaochaguliwa kwa kuwapa ushirikiano, ili
kuongeza wanachama wapya na kukiwezesha chama kuendelea kushika dola.
Nyamka
alisema kuna kazi kubwa ya kushawishi watu kujiunga na chama na kuongeza
wanachama wapya kazi ambayo wanaifanya na wanaendelea kuifanya.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment