Mwandishi wetu, Pwani
MJI wa Bagamoyo mkoani Pwani imeelezwa kuwa unahitaji kufanyiwa maboresho makubwa ikiwamo kufanya ukarabati wa miundombinu ili uweze kuendana na kasi ya ukuaji ambao kwa sasa ongezeko la watu na ukuaji wake hauendani na mazingira halisi ya mji yenyewe.
Hayo yamelezwa na Waziri wa Elimu na Ufundi na Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa wakati akizungumza na wananchi na waasisi wa mji huo wakati wa ziara yake mkoani humo.
Amesema kunahitajika nguvu kubwa kuweza kurekebisha mji huo kutokana na hali halisi ilivyo sasa ikiwamo kufanya ukarabati wa miundombinu ili uweze kuendana na kasi ya ukuaji na ongezeko la watu.
Kawambwa amesema katika kuhakikisha hilo linafanyiwa kazi anatarajia kukaa na viongozi wa mamlaka ya mji mdogo na wadau wengine ambapo pamoja na mambo mengine watajadili mustakabali wa maendeleo ya mji huo.
Amesema atasimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo wilayani humo kwa kushirikiana na Serikali, watendaji wa halmashauri, kata na vijiji ili kuleta mabadiliko ya maendeleo ya wilaya hiyo.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment