na Dina Ismail
CHAMA cha Soka Wilaya ya Mkuranga (MDFA), mkoa wa Pwani, kimepata viongozi wake watakaokiongoza kwa kipindi cha miaka minne.
Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi mjini Mkuranga, wajumbe 46 kutoka klabu 19 wanachama hai wa MDFA walishiriki kupiga kura.
Waliochaguliwa ni Mwenyekiti, Sudi Baisi, Katibu Mkuu Issa Kivyele, ambao hawakuwa na wapinzani, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA aliibuka John Malata na mwakilishi wa klabu ni Rashid Selungwi ambaye ndiye aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
Nafasi nyingine hazikuwa na wagombea, ambapo uchaguzi mdogo utatangazwa ili kuziba nafasi zilizowazi hapo baadaye.
Mkuranga ni wilaya ya pili kati ya sita za mkoa wa Pwani kufanya uchaguzi, baada ya Kisarawe kukamilisha zoezi hilo wiki mbili zilizopita.
wilaya za Rufiji na Mafia zinatarajiwa kufanya uchaguzi wao Septemba 29, Bagamoyo Oktoba 8 na Wanawake (TWFA), Septemba 29.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment