Naibu
Waziri wa Wizara mpya ya nishati Subira Mgalu akizungumza na watendaji
wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani pamoja na wakandarasi baada ya
kukagua mradi wa REA awamu ya tatu uliopo maeneo ya sofu mlandizi
Wilayani Kibaha mkoani Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku
moja kwa ajili ya kujionea mwenendo mzima wa ujenzi.(PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Naibu
Waziri wa nishati Subira Mgalu wa kati kati akipata maelezo kutoka kwa
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto katika
alipotembelea kituo cha usambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi.
Naibu
Waziri wa Wizara mpya ya nishati Subira Mgalu akipata ufafanuzi kutoka
kwa wakandarasi wa mradi wa umeme wa REA awamu ya tatu katika eneo la
Msufini Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Naibu
waziri mpya wa Nishati Subira Mgalu akisikiliza kwa umakini maelezo
kutoka kwa Meneja wa tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto mara
baada ya kutembelea kituo cha umsambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi
ikiwa ni ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya nsihati
ya umeme
NA VICTOR MASANGU, PWANI
VIJIJI
vipatavyo 54 katika mkoa wa Pwani ambavyo wananchi wake walikuwa katika
hali ya sintofahamu kutokana na kukaa gizani kwa kipindi cha muda mrefu
hatimaye wanatarajia kupata na kunufaika na nishati ya umeme wa uhakika
ifikapo mwezi machi mwaka 2018 baada ya kukamilika kwa mradi wa
kusambaza umeme vijiji (REA) awamu ya tatu.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa wizara ya nishati Subira Mgalu baada
ya kufanya ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Bagamoyo
pamoja na Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kutembelea baadhi
ya miradi ya REA ambayo inatekelezwa kwa awamu ya tatu pamoja na
kujionea changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Pia
Magalu amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha inapeleka huduma ya uhakika
kwa wananchi wake pamona na maeneo mengine yenye kutoa huduma za kijamii
na kubainisha kuwa wanatarajia ifikapo mwaka 2021 vijiji vtote nchini
view vimefikiwa na huduma ya nishati ya umeme.
Aidha
Naibu Waziri huyo alipotembelea kituo cha uzalishaji wa umeme kilichopo
maeneo ya Mlandizi aliliagiza Shirika la ugavi wa umeme Tanesco
kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kuweza kupunguza malalamiko
ambayoyamekuwa yakitolewa na baadhi ya wananchi kuunguza vitu vyao
majumbani kutokana na tatizo la kukatika katika umeme kila mara bila ya
kutoa taarifa.
“Jamani
viongozi wangu wa Tanesco kumekuwepo na baadhi ya malalamiko ambayo
yamekuwa yakitolewa na wateja kuhusina na hii hali ya kukatika katika
kwa umeme mara kwa mara bila ya taarifa hali amabyo inasababisha wakati
mwingine wananachi hao kuunguza vitu vyao hivyo katika hili mimi
nawaomba mbadilike na mlifanyie kazi katika kuhakikisha lawama hizi
zinaondoka kabisa na nina imani mtalifanyia kazi,”alisema Mgalu.
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika la ugavi wa umeme (Tanseco ) Mkoa wa Pwani
Martin Madulu amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa REA awamu ya
tatu utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la nishati ya umeme
kwani wanatarajia kuwafikiza zaidi ya wateja 5000, na kuongeza kuwa
mradi huo umegharimu kiasi cha shiingi bilioni 5.
Meneja
Madulu aliongeza kuwa lengo la Tanesco ni kuhakikisha kwamba
wanaboresha zaidi huduma ya nishati ya umeme hususan katika maeneo ya
vijijini kwa lengo la kuweza kuwafikia wananchi wengie ambao wataweza
kupata fursa ya kutumia nishati hiyo katika kuendeshea shughuli zao
mbali mbali za kimaendeleo.
Mhandisi
mkuu ambaye anayesimamia miradi ya umeme wa vijijini (REA) katika Mkoa
wa Pwani Leo Mwakatobe amesema licha ya kujitahidi katika kunga
miundombinu mipya kwa ajili ya nishati hiyo wanakabiliwa na chanagmoto
kubwa ya kuwepo kwa baadhi ya wananchi kugoma kuhama kwa ajili ya kupata
njia ya kupitsiha mradi huo hivyo kuwapa wakati mgumu katika
utekelazaji wa majukumu yao.
“Katika
miradi hii ya kusambaza umeme vijijini kwa kweli baadhi ya maeneo bado
tunakabiliwa na changamoto kubwa ya wananchi kuwa wagumu kupisha eneo
kwa ajii ya kuweza kupata njia ya kupitisha nishati ya umeme, hivyo
inatupa wakat mgumu sana katika kufanya kazi zetu na wengi wao wanadai
fidia ya kulipwa lakini katika maradi huu hauna fidia kitu kikubwa ni
kutupa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili,”alisema Mhandisi
Mwakatobe.
KUKAMILIKA
kwa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA) katika Mkoa wa Pwani
utaweza kuvinufaisha vijiji vipatavyo 154 ambavyo baadhi ya vingine
vilishapatiwa umeme huo katika awamu ya kwanza pamoja na ya pili.
0 comments:
Post a Comment