Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa sherehe za kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya mikopo ambayo iatawasaidia katika kuendeshea shughuli zao za biashara pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.
Mkuu wa Wilaya Kisarawe Happiness Seneda aliyesimama akizungumza na vikundi vya wajasiriamali kutoka kata mbali mbali katika halfa fupi ya kukabidhiwa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili mkopo wa kuwawezesha kiuchimi.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe Mussa Gama akizungumza na vikundi vya wajasiriamari hao hawapo pichani kabla ya kukabidhiwa hundi hiyo ya kiasi cha shilingi milioni 102 kwa ajili ya kuwawezesha mikopo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU.
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
HALMASHAURI
YA wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi
za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kuwa na uchumi wa
viwanda imetoa kiasi cha shilingi milioni 102 kwa vikundi vya
wajasiriamali vipatavyo 49 vya wakinamama,vijana pamoja na walemavu
kwa lengo la kuweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao mbali mbali za
biashara mbali mbali ikiwemo na kuwawezeha ili waweze kujikita zaidi
katika kujenga viwanda vidogo vidogo.
Akizungumza
katika halfa fupi ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyohuduriwa na
viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa vikundi hivyo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama
alisema kwamba fedha hizo za mikopo zimetolewa kwa vikundi hivyo
kutokea kata zote 17 ambapo zimetokana na makusanyo ya mapato ya ndani.
Mkurugenzi
huyo alibainisha kuwa kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo
na kuweza kukuza uchumi wa nchi kutokana na kuweza kuwapa fursa
wajarisiamali hao kupania wigo wa kibiashara pamoja na kuanzissha
viwanda vingine vidogo vidogo ambayo vitaweza kuongeza upatikanaji wa
ajira mpya na kupunguza wimbi la umasikini.
“Kwa
kweli sisi kama halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe tumejipanga kuweka
mipango madhubuti katika kuviwezesha vikundi vyetu vya ujasiriamali kwa
kutumia fedha zetu ambazo zinatokana na makusanyo ya mapato ya nadani,
hivyo vikundi hiivi ni moja ya mipango yetu katika kuhakikisha ile
asilimia 10 iliyotengwa inawafikia walengwa na kuweza kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo,”alisema Mkurugenzi huyo.
0 comments:
Post a Comment