Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kiramba kata ya Nyamato wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga na kuwaahidi kushugulikia mgogoro wa wafugaji na wakulima.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Bigwa wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wanakijiji wa Mkiu wakati wa ziara yake ya Jimbo la Mkuranga na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akisalimiana na wanakijiji baada ya kuwasili kwenye ziara yake katika Jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
NAIBU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema atahakikishia mgogoro
wa wafugaji na wakulima katika Wilaya ya Mkuranga unamalizika kwa
kufikia makubaliano yenye kuleta tija.
Alizungumza
hayo wakati wa ziara yake katika vijiji vya Kiramba, Mkiu, Bigwa na
Kilimahewa Kusini, Naibu Waziri ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la
Mkuranga amesema kuwa mgogoro baina ya wafugaji na wakulima upo siku
nyingi ila kwa sasa anataka kuhakikisha analitatua kabla kufikia kuleta
madhara kwa wananchi wa maeneo hayo.
Ulega
amesema kuwa, tatizo la mgogoro wa Wafugaji na wakulima lipo siku
nyingi hata kabla ya yeye kuteuliwa na amepita kwenye vijiji hivyo na
ameendelea kuliona ila kwa ushirikiano baina yake na Halmashauri ya
Manispaa ya Mkuranga watafanikiwa kutatua mgogoro huo ambao bado haujawa
mkubwa sana.
Katika
Kijiji cha Kiramba na Mkiu, baadhi ya wananchi walitoa malalamiko yao
kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kuwa wafugaji
waliokubaliwa na kijiji kwa ajili ya kuleta mifugo yao kwa sasa imekuwa
kero wakiingia mpaka mashambani na kuharibu mazao yao.
Wanakijiji
hao wamelalamika kuwa wafugaji walioidhinishwa katika mkutano wa kijiji
wamekaribisha na ndugu zao ambapo kinasababisha mifugo kuwa mingi sana
na mingine kuletwa mpaka kwenye mashamba yao kwa ajili ya malisho.
Mbali
na hilo Naibu Waziri aliweza kukutana na changamoto ya barabara ya
kimanzichana kulekea Kiramba, Tipo na Mkonoge na kumuagiza Mkandarasi
kutoka Manispaa ya Mkuranga na Meneja wa TARURA kuhakikisha tatizo hilo
linamalizika kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika mwakani.
Katika
ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega ametoa mifuko ya saruji kwa Kijiji cha
Kiramba, Mkiu, Bigwa na Kilimahewa Kusini kwa ajili ya muendelezo wa
maendeleo ya kijiji humo.
0 comments:
Post a Comment