Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMANDA
wa polisi mkoani Pwani ,kamishna msaidizi wa polisi (ACP ) Jonathan
Shannaakizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani.
Baadhi ya maofisa wa Polisi wakiwa katika mkutano huo.
Na Mwamvua Mwinyi
KAMANDA
wa polisi mkoani Pwani ,kamishna msaidizi wa polisi (ACP ) Jonathan
Shanna ,amesema amejipanga kupambana na wahalifu mbalimbali kwa kuwasaka
uvungu kwa uvungu ,ficho kwa f
Aidha amewataka wakulima na wafugaji kuheshimiana kwa lengo la kuondoa migogoro baina yao .
Mbali
na hayo amewaonya madereva wa vyombo vya moto ikiwemo mabasi yaendayo
mikoani na magari madogo kutii sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara barabara kuu ya
Dar as salaam -Morogoro .
Akizungumza
na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi Mkoani Pwani pamoja na
waandishi wa habari Mkoani hapo,kamanda Shanna ,aliomba ushirikiano kwa
askari polisi,waandishi hao pamoja na jamii .
Shanna alieleza kwamba ,atakwenda kitanda kwa kitanda ,pori kwa pori kuhakikisha wanapunguza matukio ya kiuhalifu .
Alisema
yeye ni mgeni lakini ni mtu wa kazi alitaka ushirikiano kwa askari wa
jeshi hilo mkoani hapa na wananchi baada ya kuchukua nafasi ya kamishna
msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga aliyehamishiwa mkoa wa kipolisi
Rufiji ambao utakuwa na wilaya za Rufiji, Mkuranga, Kibiti na Mafia .
“Baada
ya kugawanyika kwenye utoaji wa huduma za Kipolisi na sisi Mkoa wa
Pwani kubaki na Wilaya za Kipolisi Chalinze na Mlandizi, na Wilaya za
Kiserikali Bagamoyo, Kisarawe, na Kibaha”alisema kamanda Shanna.
Katika hatua nyingine ,Shanna alisema Mariamu Omari (31) mkazi wa Muharakani Kwamatias, wilaya ya Kibaha amefariki dunia baada ya kuuwawa na watu wasiojulikana .
Alisema
mwili wa mwanamke huyo ulikutwa nje ya nyumba anayoishi mbele kidogo
umbali wa mita 40 akiwa anavuja damu nyingi sehemu za usoni na jereha
kichwani upande wa kushoto.
Kamanda
Shanna alieleza kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani Pwani
linafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaweza kuwabaini
waliojihusisha na tukio hilo .
Aliwataka wananchi watoe ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
0 comments:
Post a Comment