Kamanda wa Polisi mkoani
Pwani Jonathan Shana akizungumza kuhusu tukio la mauaji ya mwanamke asiyejulikana aliyekutwa amefariki dunia jana usiku na kutangaza mapambano makali ya kuwatia nguvuni wahalifu
Kamanda Shana amesema kuwa mwili wa
mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Omari (31) ulikutwa nje
ya nyumba anayoishi mbele kidogo umbali wa mita 40 akiwa anavuja damu
nyingi sehemu za usoni na jereha kichwani upande wa kushoto huku muuaji
akiwa bado hajafahamika.
"Kufuatia tukio hili jeshi la polisi mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaweza kuwabaini waliojihusisha na tukio hilo, Pia wananchi wanatakiwa watoe ushirikiano kwa kuwafichua wahalifu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pamoja na hayo Kamanda Shana amewatahadharisha watu wote wanaojishughulisha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani jeshi limejipanga kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

0 comments:
Post a Comment