Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akimuuliza maswali Dereva wa basi la Safari Express linalofanya safari
zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara
ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani.
Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kushoto) kumuondoa Mkuu
wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na
achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na
kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari
zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara
ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani.
Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama
Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za
kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufanya ukaguzi wa magari na kusimamia
sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa
maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Jonathan
Shana, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo
cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama
Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani, Abdi Isango (wapili kushoto) katika
nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa
kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
akizungumza na waendesha bodaboda wa Mji wa Chalinze, wakati kiongozi
huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha
Maili Moja, Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani. Masauni aliwataka
waendesha boda boda hao kufuata sheria za barabarani na pia
alimuagiza Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili
kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani
katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa
kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani
mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha Kibaha
Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza kituoni
hapo. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) kumuondoa Mkuu
wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) mkoani humo katika nafasi hiyo na
achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufuata maelekezo
aliyowahi kupewa ya kukagua magari na kusimamia sheria za usalama
barabarani.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa
maelekezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) wakati alipokua anazungumza na
askari wa usalama barabarani katika eneo la Sanzale, Bagamoyo. Masauni
alifanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Mabasi Kibaha, Chalinze pamoja na
kukagua barabara hadi kufika mjini Bagamoyo.
Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka
Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama
Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu
kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani
humo.
Masauni
akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika
Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake
aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.
“Mwaka
jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna
mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi
haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari
hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,” alisema Masauni na
kuongeza kuwa;
“RTO
ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika
nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki
kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni
mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani
Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye
Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
Akiwa
mjini Chalinze, Masauni alizungumza na waendesha bodaboda na kuwapa
maelekezo kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani kwa
kutobeba mishikaki, uvaaji wa kofia ngumu na pia kufuata sharia zote za
usalama barabarani.
“Mmenihakikishia
kwa wale ambao hamkua na kofia ngumu kuwa mkitoka hapa mtakwenda
kuzitafuta, hakikisheni mnafanya hivyo kwa usalama wenu pamoja na abiria
mnaowabeba, ipendeni kazi yenu kwa kuheshimu sharia za usalama
barabarani,” alisema Masauni.
Akiwa
njiani kuelekea Chalinze mpaka Bagamoyo, Masauni ambaye gari yake
ilitolewa namba zinazomtambulisha nafasi yake (NWMNN), na kuweka namba
za kawaida ili kujua kama akiendesha kwa mwendokasi barabarani matrafiki
watalisimamisha gari lake, hata hivyo askari wa usalama barabarani
sehemu kubwa hawakuwepo barabarani na pia waliokuwepo hawakuweza
lisimamisha gari lake.
Kutokana
na hatua hiyo, Masauni akagundua kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanywa na
matrafiki mkoani humo kwa kutofanyakazi zao kwa umakini, na kwa uzembe
huo ndio chanzo cha ajali zinazotokea barabarani mara kwa mara.
Akizungumza
na matrafiki wilayani Bagamoyo ambao walifanya uzembe huo, aliwataka
wabadilike haraka iwezekanavyo kufuata wajibu wao, na pia alitoa siku
tatu kuhakikisha wanawakamata waendesha bodaboda wote ambao wanavunja
sheria za usalama barabarani, na pia baada ya operesheni hiyo apewe
ripoti haraka iwezekanavyo, na muda wowote atafanya ziara ya kushtukiza
kuona kama maelekezo hayo wameyafanyia kazi.
“Bodaboda
nimeziona nyingi zinapita hapa zikiwa zinavunja sheria, madereva na
abiria hawajavaa kofia ngumu, na nyie mpo hapa mnaziangalia, sasa
nawaagiza mtekeleze maagizo niliyotoa na pia sio nyie tu bali nchi nzima
wahakikishe wanayakagua magari pamoja na bodaboda, na atakaepuuza
atutacheka nae, tutapambana nae,” alisema Masauni.
Kwa
upande wake Kamanda Msilimu, alisema ameyapokea maagizo yote na
atahakikisha anayafanyia kazi ipasavyo kwa kuwasimamia matrafiki wote
nchini kwa umakini mkubwa.
0 comments:
Post a Comment