Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wataalam wa ujenzi wa daraja la Kologombe linalounganisha Kijiji cha Gwata na Dololo wilayani Kisarawe. |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za mji wa Kisarawe. |
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na walimu wa sekondari Gwata alipotembelea kukagua ujenzi wa madaraja wilayani Kisarawe. |
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka
wakandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara na majengo katika
halmashauri zote nchini kuzingatia mikataba ya ujenzi, huku akiwaonya
tabia ya kuchelewesha kukamilisha miradi kwa wakati.
Jafo aliyasema hayo katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya barabara na madaraja wilayani Kisarawe.
Amesema Ofisi ya Rais, Tamisemi haitofumbia macho wakandarasi ambao wameshinda tenda za ujenzi na kuonesha uwezo mdogo.
“Pia
hatutafumbia macho ucheleweshaji wa miradi bila sababu yeyote ya msingi
kinyume na matarajio yaliyoainishwa ndani ya mkataba,”amesema Jafo
Naibu
Waziri Jafo katika ziara zake hivi karibuni ikiwemo ujenzi wa daraja la
Twangoma lililopo wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam amekuwa
akisisitiza wakandarasi kuzingatia ubora wa madaraja yanayojengwa
nchini ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.
Jafo
amemaliza ziara yake leo wilayani Kisarawe na anatarajia kuendelea na
ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro, Songwe, Njombe, Singida, Tabora,
Kagera, Mwanza na Mara.
0 comments:
Post a Comment