Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Wazee wastaafu wa Kibaha Mjini mkoani Pwani kinatafuta Sh
mil 400 kwa ajili ya kujenga kituo cha wazee kwenye eneo lao lililopo
Chalinze wilayani Bagamoyo.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama hicho, Acquiline Ndungwi, wana malengo
ya kujenga kijiji cha kisasa cha wastaafu kitakacho gharimu fedha hizo
hadi kukamilika.
Ndungwi alisema, kwa sasa wanaendelea kutafuta wadau mbalimbali ambao
watawezesha kusaidia kufikia malengo hayo katika eneo lao hilo la ekari
100.
“Kwa kuwa tayari tuna fedha kidogo tunataraji ujenzi huo kuanza
wakati wowote kuanzia sasa, kwani taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa
tayari zimekamilishwa na kinachobaki ni kupata fedha kwa ajili hiyo,”
alisema Ndungwi.
Alisema, katika harambee iliyofanyika ili kupata fedha za ikuanza
ujenzi huo, wameingiziwa zaidi ya Sh mil 12 katika taasisi ya kifedha ya
ACB, na Sh mil 1.5 zilizotolewa ahadi hivyo jumla kuwa na Sh mil 13.5.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama hicho, Josephina Protas
aliwaomba wadau mbalimbali mkoani Pwani na nje ya mkoa huo kujitokeza
kushirikiana nao kufikia mipango hiyo itakayoinua wazee kimaendeleo.
Protas alisema mafanikio yao katika mpango huo yatawafanya waweze
kujitafutia kwa kujishughulisha na miradi mbalimbali, badala ya kusubiri
kuomba misaada. Chama hicho kilianza mwaka 2014 kikiwa na wanachama 15
na sasa kina wanachama 30.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment