Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Mkoa wa Pwani imeziomba
Halmashauri za mkoa huo kuwatengea maeneo ya biashara kulingana na aina
ya biashara kuepusha migogoro kati ya wafanyabiashara moja na nyingine,
wanaoweza kutenganishwa kulingana na aina ya biashara zao.
Akizungumza na gazeti hili jana mjini hapa, Mwenyekiti wa JWT Mkoa,
Abdala Ndauka alisema baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakigombana
kuwania nafasi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao za kila siku.
Ndauka alisema maeneo mengi kwenye Halmashauri za mkoa huo hayana
sehemu za kufanyia biashara kwa kutegemea na aina ya biashara husika,
hali inayowazuia kufanya biashara kwa uhuru.
“Kuna ukosefu mkubwa wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya aina ya
biashara hali inayofanya wafanyabiashara wagombanie maeneo kwa ajili ya
biashara zao pia hakuna masoko yenye hadhi kwa ajili ya
wafanyabiashara,” alisema Ndauka.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment