Home » » CBE yatoa msaada wa mashuka 90 kwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga

CBE yatoa msaada wa mashuka 90 kwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga


Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana wilayani Mkuranga kama sehemu ya Chuo hicho kuadhimisha miaka 50 toka kianzishwe mwaka 1965.
Baadhi ya Wauguzi na wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga wakiangalia moja ya shuka kati ya mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na chuo hicho katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga ikiwa ni sehemu ya mpango wa chuo hicho kutoa huduma kwa jamii.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) kabla ya kukabidhiwa msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na CBE kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga jana.
Jengo la Wodi ya watoto la hospitali ya wilaya ya Mkuranga litakalonufaika na msaada wa mashuka yaliyotolewa na chuo cha CBE jana. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa