WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe,
Jumamosi ya wiki hii anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya
pili ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB).
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa UB, Happiness Katabazi, Waziri Membe
ndiye atakuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ambayo yatafanyika Hoteli
ya Kiromo View Resort kijijini Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani.
Katabazi, alisema wahitimu 99 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti katika
ngazi ya Shahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Diploma na cheti.
Katika hatua nyingine, juzi Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal,
alishindwa kuhudhuria sherehe za uwekwaji wa jiwe la msingi wa makazi ya
kudumu ya UB, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa makao makuu ya UB
kijijini hapo ambapo ujenzi ukikamilia majengo hayo yatakuwa na uwezo
wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 5,000 yaliyopaswa yafanyike Kiromo
kutokana na kubanwa na majukumu mengine ya kitaifa na kuomba apangiwe
tarehe nyingine.
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment