Home » » SPIKA EALA AUNGA MKONO HIFADHI YA MAZINGIRA

SPIKA EALA AUNGA MKONO HIFADHI YA MAZINGIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SPIKA wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Dk Margaret Zziwa ameipa heshima Tanzania kwa kupanda mti aina ya mtiki ikiwa ni ishara ya kuthamini, kuhifadhi na kutunza mazingira nchini.
Alipanda mti huo jana kwenye Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mjini Bagamoyo.
“Huu ni utaratibu wetu na ni azimio tuliojiwekea kama EALA kupanda miti kila tunapoenda kufanya mkutano katika nchi washirika ndani ya jumuiya yetu ili kuwasisitiza wananchi umuhimu wa kutunza mazingira,” alisema Dk Zziwa.
Dk Zziwa ambaye pamoja na wabunge wenzake walitembelea chuo hicho, alisema imekuwa desturi ambayo pia ni utaratibu waliojiwekea Bunge hilo kupanda miti kila wanapokuwa na mkutano kila mwaka katika nchi washirika ambapo mikutano hiyo hufanyika kwa mzunguko ndani ya jumuiya.
Kwa mujibu wake, mti huo ilikuwa upandwe Dar es Salaam lakini waliamua iwe Bagamoyo ambako pamoja na kutembelea TaSUBa, walijionea hazina ya historia Afrika Mashariki iliyopo katika Mji mkongwe wa Bagamoyo.
Aidha, Dk Zziwa amempa jukumu Mbunge wa EALA kutoka Tanzania ShyRose Bhanji la kutembelea taasisi hiyo na kujionea hali ya miti waliyoipanda wakati wa ziara yao inavyoendelea kumea na kutoa taarifa mara kwa mara katika Bunge hilo.
Chanzo;Habari Leo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa