Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Tecnolojia Prof.Makame Mbarawa akifungua mkutano huo unao husisha majadiliano ya wataalamu wa afya katika kuingia mfumo wautoaji huduma y a afya kwa mtandao
Dr.Kisanga akitoa maelezo katika mkutano huo wamatibabu mtandaoni
Peter Ulanga CEO & Fund Manager: UCSAF akiwa anatoa hutoba fupi kuhusiana na matibabu kwa njia ya mtandao katika mkutano wa majadiliano kwa madaktari
madaktari wakifuatilia kwa umakini ufunfuzi wa mkutano wa kujadili matibabu mtandao
Baadhi ya madaktari mbalimbali kutoka mikoa tofauti tofauti waliweza kuhudhuria mkutano huo
Picha ya pamoja mara baada ya kufungua mkutano huo Prof.Makame Mbarawa akiwa na wataalamu wa Afy.
Wakati dunia inaendelea kuwa kijiji jopo la madaktari limeendelea kutuweka karibu na kuhakiksha tunapata huduma zilizo bora na za uhakika kwa wakati kupitia (UCSAF) Universal Communications Service Access Fund's ambo wameweza kuandaa na kutambua umuhimuwa matibabu hapa nchini kwa kuanzisha matibabu kwa njia ya mtandao ambapo kipengere hikcho kitamsaidia mtanzania kuweza kutibiwa magonjwa mbalimbali hususani magonjw yale yenye wataalamu wachache hapa nchini mfano magonjwa ya moyo namengine mengi.
Prof.Makame Mbarawa Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Tecnolojia amezindua mkutano wa siku mbili wa madaktari ambapo wamekutana kutoka mikoa mbalimbali ilikuweza kujadili kwa kina katika mfumo huo wa matibabu mtandao madaktari hao ambao wataweza kuelezana mambo mbalimbali na changamoto katika matibabu mtandao na kuweza kufanya utatuzi ili huduma iweze kuanza mapema iwezekanavyo
Akifungua mkutano huo katika hotuba yake amesema hospitali zote za rufaa zimeweza kupata huduma hii na kugawiwa fifaa na hivi karibuni vinaenda kuanza kufanya kazi alizitaja hospitali zilizo pewa kipaumbele katika kuanza kutoa huduma hiyo ni pamoja na hospitali ya Taifa ya muhimbili, Mbeya,Bagamoyo,kcmc na nyingine
pia alisema kuwa hospitali zote za wilaya zitashugulikiwa ili kuweza kupata huduma hizi kwa wakati ili kupunguza ghalama na kumrahisishia mtaalamu ambapo mtaalamu huwa na wagonjwa wengi kwa wakati mmoja hivyo kwakuanzaisha huduma hii kutakuwa na uafadhari wa kufanya kazi kwa ufasaha na makini
Mwisho alitoa rai kwa wamiliki wa hospitali zote hapa nchini kujiunga na huduma hii kwani inafaida kwa wote aliongeza kwa kusema wameingia makubaliano na mtandao wa simu wa vodacom ili waweze kufunga huduma ya network katika hospitali ya muhimbili iliwagonjwa waweze kupata huduma hiyo bure na kuweza kuwasiliana na watu mbalimbali ilikuwea kuwajulisha hali zao na huduma hiyo iko mbioni hivyo mashirika mengine ya mitandao ya simu kushauliwa kwenda katika hospitali mbalimbali na kuiga mfano kwa shirika hilo maana huko ndiko kujitangaza na kuwateka watu watakao fika maeneo hayo ili kuwa na biashara nzuri katika jamii.
0 comments:
Post a Comment