Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla amesema
ili kuimarisha ustawi wa jamii na kudumisha amani, taasisi mbalimbali
zinapaswa kuunga mkono juhudi zifanywazo na Serikali ya Tanzania katika
kuboresha huduma muhimu kwa jamii.
Alisema huduma hizo ni pamoja na elimu, afya na upatikanaji wa maji safi na salama.
Aliyasema hayo juzi mjini hapa baada ya kuzindua
Kituo cha Sara na Utamadunisho cha Mlandizi (Mlandizi Spiritual Centre)
kilichojengwa katika Kijiji cha Dutumi.
Kituo hicho kimejengwa na Shirika la Mapadri wa
Maisha ya Kitume wa Kazi ya Roho Mtakatifu, chini ya ufadhili wa Padri
Robart Anhof kutoka Italia kwa kushirikiana na wadau wengine.
Alisema maendeleo ya wananchi yatapatikana iwapo
watapatiwa huduma zote za muhimu, hali ambayo itawasaidia pia kujinasua
kutoka katika lindi la umaskini.
Naye Mkuu wa Shirika la Kazi ya Roho Mtakatifu
Kanda ya Afrika, Padri Beatus Urasa alisema kituo hicho kimejengwa kwa
lengo la kuwaimarisha watu kiroho, kimwili, kijamii na kielimu kulingana
na hali ya mazingira na utamaduni wa kiafrika.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment