Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Familia mbili za Kitongoji cha Wamba, Kata ya Kandawale wilayani
Kilwa zimekutana na kumaliza kinyemela kesi ya kubakwa mwanafunzi wa
darasa la saba Shule ya Msingi Ngarambe na kumsababishia ujauzito.
Mratibu wa elimu wa Kata ya Ngarambe, Daudi
Sendaro alisema wazazi wa pande hizo mbili walikutana kumaliza mgogoro
huo, lakini waliposhtukiwa walimtorosha mbakaji.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Rajabu Banda alisema
mwanafunzi huyo alikuwa anasoma darasa la saba na ni miongoni mwa
wanaotarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa kuwa ana
sifa zote.
Mwenyekiti wa kamati ya shule, Edwina Kinawiro
alisema wametoa taarifa kwa mratibu wa elimu wa Kata ya Ngarambe kwa
ajili ya hatua zaidi.
“Sijajua kama ataruhusiwa kufanya mtihani akiwa mjamzito,” alisema Kinawiro.
Mratibu huyo, Daudi Sendaro alisema ikiwa ujauzito
wa mwanafunzi huyo ni mdogo, atafanya mtihani huo na akifaulu atarudi
shuleni kuendelea na masomo lakini kama ujauzito wake ni mkubwa
atazuiwa.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment