Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chalinze. Raia 47 wa Ethiopia wamekamatwa katika Msitu wa Mwidu ulioko eneo la Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Wanatuhumiwa kuingia nchini kinyume cha sheria
ambapo kati yao, 11 walikutwa wakiwa hawajiwezi kutokana na kutapika
hivyo kulazimika kupelekwa katika Kituo cha Afya cha Chalinze kwa
uchunguzi na matibabu ya awali.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Athumani
Mwambalaswa alisema waliwatia mbaroni baada ya kupata taarifa kutoka kwa
wasamaria wema.
“Tuliletewa taarifa na wasamaria wema kuwa kuna
kundi la watu wamejificha kwenye msitu huo na hali zao zinaonekana
kudhoofu,” alisema Mwambalaswa.
Hata hivyo, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha
kuwa watu hao walitelekezwa na waliokuwa wakiwasafirisha, “Tunaendelea
kuwashikilia mpaka hapo Idara ya Uhamiaji itakapochukua hatua nyingine
za kisheria,” alisema.
Akizungumzia afya za watu hao, Dk Masam Faustine
wa kituo hicho cha Chalinze, alisema zinaendelea vizuri baada ya
kuwapatia huduma ya kwanza. “Tulipowafanyia uchunguzi wa awali tulibaini
baadhi yao sukari ilikuwa imeshuka sana na wengine walikuwa na
malaria,” alibainisha daktari huyo.
Alisema licha ya hali zao kuendelea kuimarika, lakini mpaka jana walikuwa bado wamelazwa kituoni hapo.
Akielezea walivyoingia nchini kutokea Ethiopia,
mmoja wa wahamiaji hao ambaye ndiye pekee aliyeweza kuzungumza lunga ya
Kiingereza, Dasaliane Nune, alisema wametoka nchini kwao kwa lengo la
kwenda Afrika Kusini kutafuta kazi.
Alimtaja raia mmoja wa Ethiopia anayeishi Mombasa, Seleman Said kuwa ndiye aliyewashawishi kwenda Afrika Kusini kutafuta kazi.
Alidai kuwa aliwaambia kuwa huko kuna fursa tofauti na Ethiopia ambako kuna vita vya mara kwa mara
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment