Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkimbiza mwenge kitaifa, Rachael Kassanda
Alizindua miradi hiyo katika kijiji cha Mkiu ikiwamo mnada na
matenki ya maji katika kijiji cha Kiramba, katika shule ya msingi
Kimanzichana na maabara katika shule ya sekondari Tambani.
Alisema lengo la kuizundua miradi hiyo ni kuwasaidia wananchi kupata maendeleo na kuwaongezea kipato.
Akiwahutubia wakazi hao aliwataka wajitokeze katika kuchangia maoni
ya upatikanaji wa katiba mpya ambayo itawasaidia kupata haki katika
mambo mbalimbali yanyoizunguka jamii.
Alisema bila ya kujitokeza katika masuala ya katiba na kutoa maoni
wanaweza kupata katiba ambayo italalamikiwa kutokana na kutokuwa na
mahitaji yao.
Aliwataka vijana kujituma kwa kufanya kazi ambazo zitawaingizia
vipato badala ya kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akizungumzia ugonjwa wa Ukimwi, Kassanda alisema kuwa hauna kinga
na umeteketeza idadi kubwa ya vijana ambao ndiyo taifa la kesho na
kuwataka vijana kutoshiriki ngono zembe na kujenga utamaduni wa
kuangalia afya zao mara kwa mara.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mercy Sila, ambaye aliupokea mwenge huo katika
kijiji cha Njopeka ukitokea Rufiji, alisema lengo la kuzindua miradi
hiyo ni njia mojawapo ya kutumiwa na wakazi wa wilaya hiyo kwa ajili ya
kuwaletea maendeleo, sambamba na kuwaongezea kipato.
Mwenge huo baada ya kuzindua miradi katika Wilaya hiyo, umekabidhiwa na Sila katika Wilaya ya Kisarawe.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment