Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI wa Kata ya Pangani na Maili Moja katika Halmashauri ya Mji
wa Kibaha, wamewazuia Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuweka
mawe katika maeneo yao kabla hawajalipwa fidia.
Maeneo hayo yamemegwa kutokana na upanuzi wa barabara ya Tamco-Mapinga.
Diwani wa Maili Moja, Andrew Lugani, akiaambatana na Mwenyekiti wa
Serikali ya Machinjioni, aliwaambia waandishi wa habari kuwa
anashangazwa kuona Tanroads wanaweka mawe kabla ya kukamilisha taratibu
za kulipa fidia.
Lugano alisema tathimini katika eneo hilo imeshafanyika na kinachosubiriwa kwa Tanroads ni kulipa fidia kwa wananchi hao.
Akizungumzia suala hilo, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani, Tumain
Sarakikya, alisema suala lao linashughulikiwa na litafanyiwa kazi muda
wowote kuanzia sasa.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment