Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Harakati za usajili zimeongezewa nguvu baada ya Kampuni ya Azam
Media kutoa Sh462 milioni kwa ajili ya maandalizi ya klabu za Ligi Kuu
Bara msimu ujao utakaoanza Agosti 23.
Kutoka kwa fedha hizo katika wakati huu ni ahueni
kwa klabu nyingi hasa ndogo ambazo zimekuwa hazina fedha za usajili na
hata za maandalizi yao.
Usajili wa wachezaji wengi makini mara nyingi
hufanywa na klabu kubwa zikiwamo Yanga, Azam na Simba huku klabu ndogo
kwa miaka mingi zikiwa za mwisho huku zikisajili wachezaji wa kawaida
kutokana na kukosa fedha.
Dirisha la usajili wa Ligi Kuu Bara litafunguliwa
Juni 15 na kwa wa mujibu wa Ofisa wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga
alisema fedha hizo ni za awamu ya kwanza ya fedha zinazotolewa kwenye
udhamini wa Azam Media ambapo kila timu inapata Sh25 milioni katika
fedha za awamu ya kwanza.
Ofisa mtendaji mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington
alisema fedha hizo zimetolewa mapema ili kusaidia maandalizi ya klabu
za Ligi Kuu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ulioanza
msimu uliopita.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment