Home » » KIDOGOZERO WAHITAJI HUDUA YA MAJIHARAKA

KIDOGOZERO WAHITAJI HUDUA YA MAJIHARAKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kijiji cha KidogozeroWAKAZI wa Kijiji cha Kidogozero, Kata ya Vigwaza, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, wameuomba uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kumsimamia mkandarasi aliyepewa jukumu la kusambaza maji kwenye kijiji hicho kwani hadi sasa hakuna dalili ya kupata maji.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Omary Mmanga, alieleza hayo hivi karibuni alipozungumza na waandishi wa habari kijijini hapo na kusema wakazi wa kijiji hicho hivi sasa wanalazimika kutumia maji ya madimbwi baada ya kumalizika kwa mvua za masika.
Alisema hali hiyo imekuwa tisho kwa wakazi wake, kwani maji hayo yamekuwa yakiwasababishia magonjwa ya tumbo, hivyo ameuomba uongozi wa halmashauri ya wilaya kuwa karibu na mkandarasi ili aweze kuukamilisha mradi huo kwa wakati.
Wakazi wa kijiji hicho; Habiba Msandawe, Ally Mumule na Zurufa Yussuf, walisema wanalazimika kutumia maji hayo na ya visima ambayo si salama
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa