Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MFUMO wa baadhi ya taasisi za fedha kutoa mikopo bila elimu kwa
wanaokopa ni moja ya vyanzo vinavyochangia wanaokopa kushindwa kutumia
mikopo hiyo kwa malengo waliyokusudia.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Simka, Lucas Mwamfupa, alibainisha hayo
wilayani hapa mwishoni mwa wiki alipozungumza na waandishi wa habari
na kusema elimu ya mara kwa mara kwa wanaochukua mikopo inasaidia
kuwakumbusha lengo la fedha wanazochukua.
Mwamfupa alisema baadhi ya taasisi zinazotoa mikopo zimekua
zikishindwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo
wanaochukua mikopo, hali inayosababisha wengi wao kushindwa kurejesha
na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mkurugenzi huyo alisema katika kampuni yake hakuwahi kupata tatizo la
mteja wake kukimbia na fedha, kushindwa kurejesha mikopo yao kwa
wakati kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kuwapa elimu mara kwa mara
na pia kuwaelimisha kuhusiana na athari za mikopo kabla hawajachukua.
“Tumekuwa na utaratibu katika kampuni yetu, kwa kuwaelimisha wateja
wetu athari za kukopa na hii imesaidia wanaokopa kutokimbia na fedha
ama kushindwa kurejesha fedha wanazokopa” alisema.
Katika mji wa Mlandizi, kampuni hiyo imeanza kukopesha wajasiriamali
13, kwa kutoa sh milioni 26 ikiwa ni baada ya kuwapatia elimu ya awali
kabla hawajakabidhiwa mikopo yao.
SIMKA ilianzishwa mwaka 2008, na sasa ina wajasiriamali 700 ambao
wamenufaika na mikopo ya zaidi ya shi bilioni 1.7 katika maeneo ya
Mafia, Kibaha, Kisarawe na Bagamoyo kwa mkoa wa Pwani, mkoa wa Dar es
Salam wilaya zote, Mbeya katika maeneo ya Rungwe na Kyela.
chanzo :Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment