Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKATI mwili wa askari
polisi mwenye namba, D 9887 Koplo Joseph Ngonyani wa Kituo cha Polisi
Mkamba, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani ukisafirishwa leo kwenda mkoani
Songea baada ya kuuawa na watu ambao wanadhaniwa kuwa jambazi, majeruhi
mmoja kati ya wawili Venance Francis ambaye ni mgambo, naye amefariki
dunia.
Francis ambaye naye
alijeruhiwa katika tukio hilo baada ya watu hao kuvamia kituo hicho cha
polisi, kupola silaha na risasi, amefariki dunia jana katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Akizungumza na Majira
jana, Bi. Annastazia Nyonyani ambaye marehemu Koplo Nyongani ni baba
yake mdogo, alisema mwili huo umesafirishwa jana kwenda Songea, Kijiji
cha Namasengo kwa mazishi.
"Tumeaga mwili saa sita
mchana, saa nane tulianza safari ya kwenda Kijiji cha Namasengo kwa
mazishi ambayo yatafanyika kesho (leo), kwa sasa bado tupo safarini,"
alisema.
Marehemu Koplo Ngonyani
alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Mkuruanga baada ya kukamtwa mapanga na watu hao ambao walivamia kituo
hicho, kupora silaha mbili aina ya SMG.
Zilaha hizo, zote
zikiwa na magazini mbili zenye risasi 30 kila mmoja na kuwajeruhi mgambo
wawili waliokuwa kituoni hapo akiwemo marehemu Francis na mwenzake
Mariam Mkamba.
Akizungumza na Majira,
Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaisha,
alithibitisha kifo cha marehemu Francis na kuongeza kuwa, mwenzake
Mkamba anaendelea na matibabu kwenye Kitengo cha Mifupa (MOI), kilichopo
hospitalini hapo.
"Marehemu alifikishwa
hospitalini hapa juzi akitokea hospitali ya Wilaya ya
Mkuranga...amefariki leo (jana), saa nne asubuhi," alisema.
Taarifa zilizolifikia
gazeti hili kutoka vuanzo mbalimbali, zinasema jeshi hilo linawashikilia
baadhi ya watu wakihusishwa na tukio hilo na wanaendelea kuhojiwa.
Awali Kamanda wa Polisi
mkoani humo, Ulrich Matei alisema jeshi hilo litahakikisha silaha zote
zilizochukuliwa na watu hao zinapatikana haraka akiwataka wananchi kuwa
wavumilivu kuhusiana na tukio hilo.
Kamishna Suleiman Kova
Katika hatua nyingine,
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limeunda kikosi maalum
cha upelelezi kwa kushirikiana na jeshi hilo mkoani ili kufuatilia tukio
la mauaji ya polisi huyo na uporaji wa silaha.
Akizingumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kamanda wa kanda hiyo, Kamishna
Suleiman Kova, alisema tukio hilo kikosi hicho kitafanya kazi usiku na
mchana ili kuhakikisha silaha zilizoporwa zinapatikana na wahusika
wanakamatwa.
0 comments:
Post a Comment