Home » » UJANGILI WAPUNGUA HIFADHI YA RUAHA

UJANGILI WAPUNGUA HIFADHI YA RUAHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

UJANGILI katika Hifadhi ya Taifa Ruaha umepungua kutokana na operesheni mbalimbali zilizofanyika katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Ruaha, Dk. Chris Timbuka, aliwaambia waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo jana kuwa kwa mwaka jana waliuawa tembo 234, lakini mwaka huu idadi imepungua na kufikia 86.
Alisema kupungua kwa uhalifu huo kunatokana na Operesheni Tokomeza ambayo waliitumia kukamata silaha na wahalifu kwa asilimia 60.
Alisema msako huo ulifanyika ndani na nje ya hifadhi ambapo silaha zilikamatwa na wengine kupelekwa mahakamani ambapo kesi zao bado zinaendelea.
“Ingawa uhalifu umepungua, lakini hali bado hairidhishi, kuna madhara kwa wanyama na jitihada zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na wizara kuongeza askari wa doria, silaha na kuwashirikisha wananchi katika ulinzi huo,” alisema Dk. Timbuka.
Alisema Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,200 ni ya kwanza kwa ukubwa Afrika mashariki na ina tembo wapatao 20,000 kuliko hifadhi nyingine yeyote na imekuwa kivutio kikubwa.
Akizungumzia utalii katika hifadhi hiyo, alisema hali ni nzuri ingawa inahitaji kutangazwa zaidi kama ilivyokuwa kwa Serengeti na hifadhi nyingine.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa