Asubuhi ya leo wanakijiji walikuwa
na sura zilizojaa bashasha na kufurahia maisha ya kijijini hapo. Shughuli
mbalimbali ziliendelea huku wengine wakifanya usafi, kubadilishana mawazo wa
,asuala mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku kwani ni moja ya miradi
inayoendeshwa katika kijiji cha Maisha Plus na wengine wakiuza maandazi
kijijini hapo ili kujipatia riziki na kujikimu na mahitaji muhimu katika
familia zao.
Wakati muuza maandazi akiendelea kufanya biashara yakatokea
mabishano ya nani anayeweza kula maandazi mengi zaidi na mabishano hayo
yakadumu kwa muda kadhaa lakini mwisho wa siku ni muuza maandazi kufaidika
zaidi kwa kuwa aliweza kuuza kwa wingi.
Baada ya hapo wanakijiji walipewa
chemsha bongo na Masoud Ali, Mkurugenzi wa DMB na mwanzilishi wa Maisha Plus ambapo
kila mwanakijijji alipata kipande cha picha ambacho kwa pamoja walitakiwa
kuviunganisha na kupata picha mbili tofauti.
Moja ya masharti ya chemsha bongo
hiyo ni kuwa matatani kwa kundi la mwisho kufanikisha kuunganisha picha hizo na
endapo zoezi hilo litashindikana basi kijijini hapo wasingeweza kuendelea na
shughuli yoyote wala kula chakula cha usiku. Hivyo basi kila kundi lilijitahidi
kuunganisha picha hizo kwa juhudi zote kwa kuhofia kuwa wa mwisho bila
mafanikiwa kwa kuwa kundi la Maisha Plus lilikuwa na vipande vya picha mbili
tofauti hali kadhalika na kundi la Mama Shujaa.
Hivyo kundi moja lisingeweza
kuunganisha na kupata picha moja iliyokamilika. Mara mwanakijini mmoja akaja na
wazo la kuunganisha picha hizo kwa kushirikiana makundi yote mawili ndipo
wakakubaliana na hoja hiyo hatimaye kufanikisha zoezi hilo. Hii inadhihirisha
kuwa bila umoja na ushirikiano hakuna mafanikio yatakayoweza kupatikana katika
jamii.
Makundi yote mawili walifurahi na
kuweza kuendelea na shamra shamra za mapishi na walishirikiana kupika pilau na
kula kwa pamoja kukamilisha furaha yao.
0 comments:
Post a Comment