Kijiji cha Maisha Plus chapata
Rais mpya ambaye huchaguliwa kila wiki. Huu ni utaratibu waliojiwekea
wanakijiji cha Maisha Plus ambapo kila wiki hupata Rais mpya atakayeongoza
kijiji hicho kwa kipindi cha wiki moja. Rais mpya wa wiki hii ni Mvano Ciza
kutoka Burundi na mama yake ndiye aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha
kijijini hapo ambaye alitakiwa kuwa Malkia. Kwa sasa Rais amepata mama mwingine
Mama Shujaa Upendo Msuya kutoka Kilimanjaro ambaye atakuwa Malkia kwa kipindi
cha wiki moja na atakuwa mshauri na muamuzi wa masuala yote kijijini.
Baada ya uchaguzi wanakijiji
waliendelea na shughuli zao za kawaida kama vile kupika, kufanya usafi na
kutembeleana. Sambamba na hayo kijiji cha Maisha plus kilipata ugeni kutoka
TAMASHA. Ugeni huo uliongozwa na Rukia Masayanyika Mratibu Mradi wa kuwafikia
wasichana wadogo walio katika mazingira hatarishi nchini akiwa na watumbuizaji
wa muziki kutoka Ujamaa Hip Hop Darasa ambao ni Nasri Kakiva, Calvin Samwel,
Neyka Stanslaus na Khamisi Ramadhani. Wanakijiji
walipata darasa kupitia kisa mkasa walichotolewa na martibu wa TAMASHA
uliochochea mjadala kuhusu ushiriki wa vijana katika masuala mbalimbali na
kufanya maamuzi kwa manufaa yao wenyewe. Imeonekana kuwa vijana hufanyiwa
maamuzi katika masuala yanayowagusa wao wenyewe inayopelekea vijana kuwa
tegemezi hapo baadaye asijue nini cha kufanya kwa kuwa wameshazoea kupewa maelekezo
kutoka kwa wazazi ama watu wanaowazidi umri. Kwa wanakijiji cha Maisha Plus
mambo ni tofauti kwani vijana wapo mstari wa mbele katika nyanja zote ikiwemo
uongozi, uchumi, utamaduni na kijamii kwa ujumla kwani tumeona vijana wakishika
nafasi mbalimbali za uongozi tena za juu na kuleta mabadiliko kijijini hapo.
Kwa upande wa burudani Nasri
Kaviva na Neyka Stanslaus walitoa burudani kwa wanakijiji cha Maisha Plus
ambapo wanakijiji walifurahia sana burudani hiyo na kutaka kujua zaidi namna
gani wanakijiji cha Maisha Plus wanaweza kuendeleza vipaji vyao ili nao waweze
kufanikiwa katika siku za usoni ukizingatia kijijini hapo tayari kuna bendi ya
Kantangaze ambapo wanaweza kuburudisha na kuonyesha vipaji vyao.
Pia siku ya leo wanakijiji
walishiriki katika kinyang’anyiro cha fedha taslimu 300,000 kwa atakaye weza
kuchukua ufunguo aliofungwa kwenye shingo ya chatu. Kila mwanakijiji alipewa
sekunde tatu kufanya zoezi hilo la kuchukua ufunguo uliofungiwa shingoni mwa
chatu kisha afungue boksi lililopo pembeni mwa chatu huyo ambapo ndani yake
kulikuwa na fedha taslimu 300,000. Zoezi hili lilikuwa gumu kwa wanakijiji cha
Maisha Plus kwani kuna ambao hawakuweza hata kumsogelea chatu huyo na wengine
walijaribu kufanya hivyo lakini hawakufanikiwa kuchukua fedha zilizopo ndani ya
boksi. Kutokana na muda uliowekwa kwa kila mwanakijiji hakuna aliyeweza kupata
fedha hizo hivyo wanakijiji wamepoteza fursa hiyo ya kujipatia fedha hizo
ambazo zingewasaidia katika kendeleza miradi yao hapo kijijini.
0 comments:
Post a Comment