Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI mkoani Pwani imeombwa kuwachukulia hatua kali za kisheria
wazazi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani kitendo
hicho kinasababisha kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo ya kupata
elimu.
Wito huo umetolewa juzi na mke wa Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM),
Selina Koka, alipozungumza na wazazi pamoja na watoto wenye ulemavu
katika ziara yake aliyoifanya katika kata wilayani hapa akiwa na lengo
la kutoa msaada kwa watoto wenye ulemavu na wale waishio katika
mazingira magumu.
Selina alisema baadhi ya wazazi wilayani hapa wamekuwa wakidaiwa kuwa
na tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu, hali inayosababisha
watoto hao kukosa haki za kupata elimu.
Alisema jamii ya watu wenye ulemavu nayo ina haki sawa kama wengine,
hivyo ni vema kama serikali itafanya kazi ya kuwawajibisha wazazi wenye
tabia kama hizo.
Selina alitoa msaada wa mchele, sukari, vifaa vya kusomea, sabuni na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 5.
Pia aliahidi kuendelea kuwasaidia walemavu waliopo katika Wilaya ya Kibaha Mjini kwa kuwapa misaada mbalimbali.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment