Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI mkoani Pwani imeombwa kuwachukulia hatua za kisheria
wazazi wenye tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu kwa kuwa kitendo
hicho kinawanyima haki za msingi ikiwemo kusoma.
Wito huo ulitolewa juzi na Mke wa Mbunge wa Kibaha Mjini Sylivester
Koka (CCM), Selina, alipozungumza na wazazi na watoto wenye ulemavu
wakati wa ziara aliyoifanya kwenye kata za Wilaya ya Kibaha kwa lengo
la kuwasaidia walemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Selina alisema baadhi ya wazazi wilayani humo wanawaficha ndani
watoto wenye ulemavu hali inayowakosesha haki na mahitaji yao muhimu.
Alisema jamii ya wenye ulemavu nayo ina haki sawa na wengine, hivyo
ni vema serikali kuwawajibisha wazazi wenye tabia hizo ili kuwa
fundisho kwa wengine na kuondoa unyanyapaa katika jamii.
Mke wa mwanasiasa huyo aliwasaidia watoto yatima, walemavu na waishio
kwenye mazingira magumu wapatao 100, vyakula mbalimbali, vifaa vya
shule na sabuni, mali zenye thamani ya sh milioni tano.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment