Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
John Pombe Magufuli
Magari yalianza kutumia barabara hiyo juzi usiku baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Dar es Salaam kutengeneza kipande kilichokuwa kimekatika.
Mhandisi wa Tanroads Dar es Salaam anayesimamia ujenzi huo, Ngusa Julius, aliwaambia waandishi wa habari waliotembelea daraja hilo kujionea maendeleo ya barabara hiyo, alisema hadi sasa eneo hilo limepokea malori 500 ya mawe na wanaendelea kujaza kwa kuwa yanatakiwa malori 700 ya mawe makubwa.
"Kwa sasa linapitika kwa upande mmoja hivyo magari yanapita kwa kupokezana, naamini hadi kesho kazi ya kujaza mawe na kusawazisha itakuwa imekamilika magari yatapishana bila wasiwasi," alisema.
Hata hivyo, Julius aliwataka madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo kuwa makini kwa kuwa kingo za barabara hazipo na kuna kina kirefu, hivyo ni rahisi kwa gari kuteleza na kutumbukia mtoni.
Daraja hilo lilikatika Aprili 13, mwaka huu kutokana na mvua kubwa iliyonyesha sehemu mbalimbali kwa siku mbili mfululizo.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment