MAOFISA
Ushirika nchini kote wameagizwa kuhakikisha wanatekeleza mfumo wa
stakabadhi ghalani ili kuimarisha vyama vya Ushirika nchini.
Rai
hiyo imetolewa juzi wilayani Bagamoyo, Mgurugenzi na Mrajisi wa Ushirika
nchini, Dkt. Audax Rutabanzibwa alipokuwa akizungumza na maofisa
ushirika wa mikoa na wilaya mbalimbali nchini.
Alisema kumekuwa na
changamoto ya vyama vya ushirika kuchukua mikopo katika benki na kulipa
wakati sio lengo la ushirika. Ushirika ni kukusanya na kutafuta soko kwa
pamoja.
"Ushirika kazi yake n i kukusanya na kutafuta soko na sio
wafanyabiashara, ushirika ukikopa unajiingiza kwenye deni ambalo analipa
mwanachama,î alisema.
Aliendelea kueleza vyama vya ushirika vya msingi na vyama vya ushirika vikuu vinapaswa kuangalia upya kazi wanazofanya.
Aliviomba
vyama vikuu visifanye kazi ya kukusanya badala yake wahusike kwenye
ngazi za juu za mnyororo wa thamani wa zao, kama vile kutafuta soko la
mazao ndani na nje ya nchi, kuogeza thamani kwenye mazao.
Alisisitiza
kuwa kazi ya kukusanya waviachie vyama vya ushirika vya msingi ili
kuepuka kuingiliana katika kazi na kuongeza gharama kwenye mnyororo wa
thamani.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Programu ya Miundombinu ya
Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF)
ililenga katika kuwaandaa maofisa ushirika nchini kuhusika zaidi katika
kusimamia vyama vya ushirika vitekeleze Mfumo wa Stakabadhi ya Mazao
Ghalani (Warehouse Receipt System) kupitia vyama vya ushirika.
Akizungumza
katika semina hiyo mtaalamu wa masoko ya kilimo kutoka MIVARF, Muhoni
Leonard alieleza kuwa kumekuwa na changamoto katika kuhusisha vyama vya
ushirika visaidie wanachama kupata masoko ya mazao ya wanachama wao,
lakini kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika na wakulima wa
chini zitakwisha.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment