BAADHI
ya vijana wahalifu waliotoka katika magerezani mbalimbali hivi karibuni
ambao kesi zao zimeisha wamebainika kuwa washawishi wakuu na
wanaoshirikiana na wahalifu na vibaka wengine kufanya matukio ya
ujambazi na wizi wa mifukoni kwenye vituo vya mabasi huko mkoani Pwani.
Akizungumzia matukio ya uhalifu sambamba na namna ya kukabiliana nao
msimu huu wa siku kuu,Kamanda wa Polisi Pwani Ulrich Matei amesema mbali
na kundi hilo pia limeibuka kundi jingine la watu ambao wanatumia fukwe
ya Bahari wilayani Bagamoyo kama njia ya panya ya kupitisha madawa ya
kulevya .
Matei amesema jeshi hilo limeongeza nguvu na mbinu mpya ya kukabiliana
na hali hiyo ambapo kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita tayari
wamewakamata wahalifu 43 waliotenda vitendo mbalimbali vya uhalifu huku
kati yao vijana waliotoka gerezani hivi karibun baada ya kesi zao
kuisha wakiwa ni zaidi ya 10.
Amesema wahalifu hao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya kukutwa
wakisafirisha magunia saba za bangi na dawa za
kulevya aina ya heroine na kokein pamoja na marobota 191 ya milungi
Kamanda huyo amewaasa wananchi kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa
mara wanapogundua kuna watu wanaowatilia shaka na siyo kusubiri hadi
wafanya uhalifu ndiyo wawatafute askari.
Katika
hatua ingine magari zaidi 400 yamekamatwa kwa makosa
mbalimbali ya barabarani katika operesheni maalumu ya kudhibiti
madereva wazembe na wasiofuata sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Matei ametaja makosa hayo ni pamoja na baadhi ya madereva
kutumia vileo wakati wakiendesha,magari mabovu 151,mwendo
kasi 67, yanayozidisha abiria 43 na yenye kupaki maeneo yasiyoruhisiwa
58.
0 comments:
Post a Comment