MKUU wa mkoa wa Pwani
Mwantumu Mahiza amesema hata sita kuwachongea moja kwa moja kwa rais Jakaya
Kikwete viongozi na watendaji wa chama na Serikali wanaoendelea kuwa kikwazo
cha maendeleo ya mkoa huo.
Mahiza alisema hayo
leo wakati akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka wilayani zote
sita za mkoa huo waliohudhuria kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC).
Amesema ubunifu
kwa mtumishi yeyote yule ni kitu muhimu zaidi katika utendaji kazi na siyo
kufanya kazi kwa mazoea hivyo ni lazima kila mmoja kupitia fani yake na dhamana
aliyopewa na Serikali abadili tabia ili kukuza pato la uchumi la mkoa
huo.
Mkuu huyo wa mkoa
amesema wapo baadhi ya watendaji wamekuwa mzigo katika kutekeleza mikakati ya
mkoa huo katika sekta za kilimo na uwekezaji hali ambayo imekuwa ikisababisha
mkoa huo kutokuendelea kwa maana ya uchumi kubaki chini na pia fursa za
wawekezaji kutotumika ipasavyo kutokana na ubunifu mbovu wa kiutendaji.
Amesema katika suala
la kilimo wilaya zimekuwa ziking’ang’ana kuhamsisha kilimo cha korosho huku
watendaji na hata wanasiasa wakijua ni zao la kudumu tena la enzi za ukoloni
ambalo kila mzaliwa wa mkoa huo analijua umuhimu wake lazima atalilima tu kama
mwana Pwani hivyo walipaswa kuhamsisha walime na mazao mengine ya muda mfupi
kwani ardhi inaruhusu.
Mkuu huyo wa mkoa wa
Pwani ameongeza kuwa yapo mazao mengine ya muda mfupi yenye masoko kama
Ufuta,alizeti,mihogo na mahindi ambayo kama watendaji na wana siasa
watawajibika kuhamasisha watu walime ni wazi kila mkazi atapata fedha za
kujikimu kwa chakula,karo za shule, matibabu na dharura zingine za kifamilia
huku wakisubiri zile za msimu wa korosho.
Akizungumzia
suala la mkoa huo kukosa maendeleo kupitia fursa za uwekezaji, Mahiza alisema
ni kwa sababu bado baadhi wa viongozi ma wilayani hawajawa wepesi wa
kuruhusu ardhi itumike na wadau hao kwani wakitoa tu muda mfupi baadae
huanzisha maandamano kupinga shughuli kuanza kwa kile wanachodai fidia.
0 comments:
Post a Comment