JUMLA ya ajali 1,452 zimeripotiwa kutoka mkoani Pwani katika kipindi cha mwaka 2013 huku zilizosababisha vifo ni 240.
Akitoa taarifa ya mwaka, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich
Matei, alisema katika ajali hizo watu waliofariki dunia ni 314 na
majeruhi ni 1,680.
Alisema Jeshi hilo pia limeweza kukusanya sh bilioni 1.6 kutokana na makosa 62,144 yaliyoripotiwa kwenye vituo vya polisi.
Kamanda Matei alisema kuwa katika makosa hayo, 61,032 yalilipiwa tozo na 1,112 madereva wake walipewa onyo.
Katika hatua nyingine, Kamanda Matei ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa
wa Pwani kuepuka kukaa katika maeneo ya ufukweni katika kipindi hiki
cha sikukuu.
Alisema katika kipindi hiki kumeelezwa kuwepo kwa upepo mkali katika
maeneo ya baharini, hivyo ni vema wananchi wakaepuka kukaa katika
maeneo hayo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment